Rais Yoweli Kaguta Museveni wa Uganda jana  amemtumia barua mwenzake wa Rwanda, Paul Kagame baada huku kukiwa ushirkiano mkia wa mbuzi kati ya nchi hizi mbili.

Barua hii  ambayo imeletwa na Waziri wa Mambo ya Nje wa Uganda, Sam Kutesa  ila maudhui yake haikujulikana.

Hata hivyo, barua hii imetumwa wakati ambapo ushirikiano kati ya hizi nchi mbili ni ovyo juu ya mashtaka ya Uganda kwamba Rwanda inafanya upelelezi nchini humo, kuwateka nyara wakimizi asili ya Rwanda na mengine.

Kwa upande mwingine Rwanda inasema Uganda inawakamata kinyume na sheria na kuwatesa kimwili Wanyarwanda  nchini humo. Pia inadaiwa kwamba Uganda inawaunga mkono wapinzani wa Rwanda.

Kila upande ulikanusha madai. Viongozi nchini Uganda walisema Wanyarwanda wanaokamatwa wanahusika na vitendo vya ugaidi na upelelezi.

Rwanda ilisema wanaokamatwa huwa katika shughuli zao za kibiashara nchini humo.

Ushirikiano kati ya Rwanda na Uganda ulianza kuwa ovyo mwaka2017 ambako Uganda ilimkamata Mnyarwanda Rene Rutagungira kwa kumshitaki kumteka nyara aliyewahi kuwa mlinzi wa Rais Kagame, Luteni Joel Mutabazi.

 

 

ACHA JIBU

Tanga igitekerezo
Andika amazina

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.