kwamamaza 7

Rais Museveni afunguka kwa nini hakumsalimia kwa vidole Rais Kagame

0

Rais wa Uganda Yoweli Museveni amefichua kuwa alivunjika mkono alipokuwa akicheza ‘Karate’ jambo ambalo lilimfanya kumsalimu Rais wa Rwanda Paul Kagame kwa kutumia mkono badala ya vidole.

Rais Museveni amesema hili baada ya kuonekana mwezi uliopita wa Machi vidole vyake vikiwa vimebandikwa vitambaa,jambo ambalo lilizusha utata mitandaoni wengi wakijiuliza nini kilichomfikia.

Baadhi ya hawa,walikuwa wakisema kuwa Rais Museveni anaugua ini na kuwa alikuwa akifanyiwa operesheni kwa jina la ‘dialysis’ kulingana na taarifa za Chimpreports.

Kupitia ukuta wake wa Twitter, Rais Museveni jana ameelezea wafuasi wake kuwa alivunjika alipokuwa mazoezini

“Tangu mwaka 1976, ninacheza Karate.Haya mazoezi hunisaidia kuishi katika hali nzuri ya afya,ninafanya mazoezi hata usiku wa manane ninapotoka ofisini” amesema Museveni

[xyz-ihs snippet=”google”]

Hii siyo mala ya kuanza Rais Museveni kuonekana hadharani akiwa katika hali hii.Ilitokea mwaka 2005 alipokuenda Marekani kumkuta Rais Obama na kumsalimia kwa kutumia mkono wa kushoto.

Wakati huo alisema kwamba alivunjika mkono kwa kuupiga kwenye gari alipokuwa alkielekea  Japani.

Subscribe to BWIZA TV to get news and song updates

click here to receive the updated news on facebook on twitter

Fred Masengesho Rugira/Bwiza.com

Leave A Reply

Your email address will not be published.

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.