kwamamaza 7

Rais makamu wa bunge akataa matokeo ya njaa

0

Mbunge pia rais makamu wa bunge Bi Uwimanimpaye Jeanne d’Arc alikataa yaliyotajwa na raia kwamba kuna njaa kali nchini Rwanda; na kuthibitisha kwamba kilichokosekana ni mazao ya kutosha kama kawaida lakini wananchi hawakukosa chakula.

Matokeo ya njaa yalitajwa hasa hasa katika jimbo la mashariki kulitokea ukosefu wa chakula kwa ajili ya jua kali, lakini viongozi wengi walikataa malalamiko ya wananchi juu ya njaa na uhamiaji wa raia katika nchi za majirani kwa sababu ya njaa.

Mbunge Uwimanimpaye Jeanne d’Arc alithibitisha kwamba hakuna matokeo ya njaa, isipokuwa ukosefu wa mazao kamili. “Kilichoonekana ni kutopata mazao ya kutosha kama kawaida,… raia hawakusumbuliwa mno ijapokuwa mwangaza wa jua ulipatikana kwa muda mrefu.”

Waziri wa kilimo na mifugu, Bi Geraldine Mukeshimana
Waziri wa kilimo na mifugo, Bi Geraldine Mukeshimana

Mnamo mwezi Julai 2016, waziri wa kilimo na mifugo Bi Gerardine Mukeshimana pia alikataa matokeo ya njaa na kusema waliohamia nchini Uganda ni kwa sababu ya kutafuta kazi siyo njaa.

[ad id=”72″]

“Wakati tunaingia kwenye shirika la Afrika ya Mashariki inamaanisha nini, nami niliwahi kupata ajira nchini Kenya. Na nyinyi mkipata kazi kama Tanzania au Kenya mtaenda. Kama ninaishi Kigali kisha nikapata kazi pale Butare nitaenda. Kwa upande wangu siyo njaa ni ukame.” Waziri Mukeshimana alisema.

Ijapokuwa mbunge huyu alikataa matokeo ya njaa, raia wengi walisaidiwa na chakula walipewa na serikali kama mahindi na maharagwe ili kusalimika; pia wakasaidiwa kupata malisho ya wanyama.

bonyeza hapa kupokea gazeti juu ya facebook juu ya twitter

Theogene U @Bwiza.com

Leave A Reply

Your email address will not be published.

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.