kwamamaza 7

Rais Kagame na mwenzake João Lourenço kujadiliana kuhusu DR Congo nchini Ubelgiji

0

Rais Paul Kagame na Kiongozi wa Umoja wa Afrika(UA) na mwenzake wa Angola João Lourenço  wanatarajia mwezi wa Juni kukutana na  viongozi wengine  nchini Ubeligiji ili kuzungumza kuhusu masuala ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo.

 Kwa mjibu wa taarifa za Jaune Afrique, ziara ya kikazi ya Rais Lourenco tarehe 3-5 Juni itamkaribisha Rais Kagame tarehe 4-6 ambako kutakuwepo mkutano wa Ulaya kuhusu Maendeleo.

Rais wa Angola, João Lourenço na mwenzake wa Ufaransa, Emmanuel Macron

Inatarajika kwamba Rais Kagame atazungumza na Mkurugenzi wa Tume ya Umja wa Ulaya, Jean-Claude Juncker, Mkurugenzi wa Tume ya baraza la Umoja wa Ulaya,Donald Tusk na Mkurugenzi wa Bunge la Umoja wa Ulaya Antonio Tajani,mfalme na Waziri Mkuu wa Ubelgiji.

Rais Kagame akiwa na mwenzake Emmanuel Maron

Haya mazungumzo nchini Ubelgiji ni baada ya yale yalioyotokea nchini Ufaransa  na Rais Macron ambayo yalizusha wasiwasi nchini DR Congo kwa madai ya kuwa Rwanda inalenga kupindua serikali ya Rais Kabila,mashtaka ambayo Rwanda ilikanusha kupitia Waziri wake wa mambo ya nje, Louise Mushikiwabo.

Fred Masengesho Rugira/Bwiza.com

 

 

 

 

Leave A Reply

Your email address will not be published.

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.