kwamamaza 7

Rais Kagame na Askofu wa kikatoliki kuhusu mchango wa kanisa katika mauaji ya kimbari

0

Katika mjadala wa kitaifa kwa mara ya 14, rais Paul Kagame na Askofu msemaji wa kanisa la kikatoliki nchini Rwanda Phillipe Rukamba wamesema kuhusu kanisa ya kikatoliki ambayo haikuomba msamaha kuhusu mchango wa washiriki wa kanisa;  mithili ya mapadili na wakristo wengine katika mauaji ya kimbari dhidi ya watutsi mnamo 1994.

Katika kikao cha pili cha mjadala huu, leo 16 Disemba 2016, baada ya masomo alitolewa na kiongozi wa tume ya kitaifa ya kupambana dhidi ya mauaji ya kimbari (CNLG) kuhusu mauaji ya kimbari na namna ya kuhifadhi maandishi yalitumiwa; mbunge Jean Marie Vianney Gatabazi alisema kuhusu kanisa ya katoliki ambayo haikuomba msamaha.

[xyz-ihs snippet=”google-pub”]

Kagame aliuliza sababu ya kanisa ya kikatoliki duniani ya kutoomba msamaha kwa niaba ya washiriki ambao walihusika na  mauaji ya kimbari dhidi ya watutsi, wakati iliwahi kuwaombea msamaha waliofanya dhambi nyingine.

Katibu mkuu wa CNLG, Dr Jean Damascene Bizimana alisema kuhusu msamaha wa kanisa ya katoriki, aliposema kwamba kiongozi mkuu wa dini hili aliwaombea msamaha waliofanya dhambi; ndipo rais Kagame alimsaidia akisema kuwa si yeye angesema kuhusu tukio hilo ndipo Askofu Philippe Rukamba alieleza zaidi.

Askofu Philippe Rukamba alieleza sababu ya kutoomba msamaha, “Sababu ni ile kwamba si kanisa iliyohusika na mauaji ya kimbari. Si kanisa ambayo ilitaarisha mauaji ya kimbari ama kutoa silaha za kutumiwa katika mauaji hayo. Ndio maana ya kuwaombea msamaha watu wetu walishiriki, wakristo;…kwa upande wetu tulifikili kwamba inatosha.”

[xyz-ihs snippet=”google-pub”]

Aliongeza kwamba wataendelea na mijadala ili kuelewa kama kuna madai kuhusu kanisa kama shirika badala ya kosa la mtu binafsi kuchukuliwa kama kosa la shirika analofanyia.

Mnamo mwezi uliopita, baraza la maaskofu liliandika tangazo la kuwaombea msamaha mapadili walihusika na mauaji ya kimbari; ijapokuwa serikali ilisema kuwa haikuridhishwa na msamaha wa kanisa la kikatoliki kuhusu mchango wa waamini wake katika mauaji ya kimbari.

bonyeza hapa kupokea gazeti juu ya facebook juu ya twitter

Theogene U @Bwiza.com

Leave A Reply

Your email address will not be published.

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.