Swahili
HABARI MPYA

Rais kagame hakuhudhuria mkutano  utakaoamua kuhusu marufuku ya kafa ulaya

Rais Paul Kagame hakuweza kuhudhuria mwenyewe mkutano wa marais wa serikali za Muungano wa Afrika Mashariki unaozungumzia kuhusu miundo mbinu na maendeleo ya kiafya,mjini Kampala Uganda.

Rais Kagame anawakilishwa na waziri wa mindo mbinu James Musoni,ila kuna taarifa  kwamba kwenye mkutano huu kutaamuriwa kuhusu ombi la kidiplomasia la Marekani kuhusu uamuzi wa hizi nchi kupiga marufuku kafa ulaya.

Inaeleweka kwa kuwa Rais Kagame hakuhudhuria kwa kuwa alimkaribisha jana Rais wa Zambia,Edgar Chagwa Lungu.Hata hivyo, taarifa za The EasterAfrican zilizotufikia ni kwamba Katibu hali  wa marekani  kwa wajibu wa uchumi na mambo kwa Afrika,Harry Sullivan alisema kwamba huu mkutano ni fursa nzuri kwa hawa marais kubadili uamuzi wao wa kupiga marufuku  kafa ulaya maarufu kama ‘Mitumba’.

Harry Sullivan alisema”Uamuzi wa hawa marais tarehe 23 ndio utakaokuwa chanzo cha lile ambalo tutafanyia hizi nchi”.

Nchi za Afrika Mashariki ziliamua isipokuwa Kenya ziliamua kupiga marufuku kafa ulaya lakini Marekani ilisema kuwa itatoa vikwazo vya kiuchumi kwani uamuzi huu ni kipingamizi kwa uchumi huru.

[xyz-ihs snippet=”google”]

Kwa upande wa Rwanda,serikali kupitia katibu hali wa wizara ya mambo ya nje,Olivier Nduhungirehe hivi karibuni alitangaza kuwa Rwanda haitabadili uamuzi wake kuhusu hili jambo hata kama baada ya huu mkutano.

Afisa huyu aliongeza kuwa uamuzi huu unalenga  kutilia mkazo maendeleo ya viwanda vya ndani.

Rwanda,Uganda na Tanzania waliamua kupiga marufuku matumizi ya kafa ulaya milele mnamo mwaka 2019.

Subscribe to BWIZA TV to get news and song updates

Bonyeza hapa kupata habari za hivi karibuni kwenye facebook na twitter

Fred Masengesho Rugira/Bwiza.com

 

 

Izindi wakunda

Tanga Igitekerezo

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.

Bwiza.com