Swahili
Home » Rais Kagame hafurahii idadi ya viongozi wanaoakilisha Rwanda katika mashindano ya kimataifa
HABARI MPYA SIASA

Rais Kagame hafurahii idadi ya viongozi wanaoakilisha Rwanda katika mashindano ya kimataifa

Rais wa Jamuhuri ya Rwanda, hakuridhika kuhusu jinsi Rwanda ilvyowakilishwa na idadi ya viongozi inayozidi ya wachezagi katika michezo ya olimpiki iliyopigwa mjini Londoni .

Katika michezo hiyo iliyopigwa mwaka 2012 Rwanda iliwakilishwa na wachezaji saba akiwemo Niyonshuti Adrien,  Uwase Sekamana Yannick, Niyomugabo Jackson, Agahozo Alphonsine, Kajuga Robert, Mukasakindi Claudette na Mvuyekure Jean Pierre.

Rais Kagame hakuelewa jinsi idadi ya viongozi ilikuwa nyingi wakati ya wachezaji ingali pungufu.

Alisema haya wakati alipokuwa akiwahotubia katika mkutano na makundi tatu ya Intore wakiwemo Impamyabigwi la Wanahabari, Imparirwakubarusha la wanaspoti, pamoja na Indatabigwi la wasaani na wanamitindo, Jumamosi tarehe 27 mai 2017.

Rais akasema “Kulikuwa na wakati mmoja nilikuwa nimearikwa kushudia michezo ya Olimpiki nchini Uingereza[…] tulikuwa tukiona wakipita waakilishi hodari wa nchi mbalimbabali, ieleweke kwamba na Rwanda ilikuwa miongoni mwa hao na niliona vilevile bendera ya Rwanda ikipepea, lakini kwa kuhesabu idadi ya wachezaji na viongozi wao niliona kwamba viongozi waliwazidi idadi, kulikuwa na wafanyakazi wa wizara mbalimbali na viogozi wengine”.

Hilo anaona ni jambo lisilofaa kuona idadi ya viongozi ikiwazidi ya wachezaji wanaowakilisha nchi katika mashindano

Aliendelea kusema ’’ Nilidhani mimi pekee nilikuwa nalidhisha kwa upande wa viongozi waakilishi, nafasi iliyokuwa inabaki ni ya wachezaji , lakini baado idadi ya viongzi walioshiriki ilikadiria asilimia tisini, tunapaswa kurekebisha tabia hii.’’

34543611720_f54f6a19a1_z

Kwa kurudi Rwanda hakukakaa kimya kuhusu hili. “Ingawa wakati niliporudi niliaarifu katika kikao cha mawaziri kuwa sikufurahia jambo hili haingekuwa sawa kushiriki katika mashindano kwa kuhudhuria tu ambapo unaona viongozi wameshiriki kwa wingi wakati wachezaji wangali wachache sana”.

Aliomba ngazi husika. Kuwa hazina budi kufuatilia kwa karibu jambo hili, kwa kutambua wanao uwezo na vipaji na kuwasaidia kujiendeleza wala si kimichezo wala si kimaisha ya kila siku.

Wenye madaraka ya kutambua vipaji hivyo wanapaswa kuvitunza na kuvifualia kwa karibu ili Rwanda isiendelee, kwa kuandaa mashindano, kufuata mkia bali iweze kuibuka mshindi pia.

[xyz-ihs snippet=”google”]

Toka mwaka 1984 hadi 2012, Rwanda iliwahi kushirikishwa na jumla ya wachezaji wapatao 42. Lakini hakuna hata mmoja alieweza kushinda medali ya aina yoyote isipokuwa Nkezabera Jean de Dieu alieweza kushinda medali katika mashindano ya paralempiki.

Rais Kagame alikumbusha kwamba haingekuwepo sababu yoyote wakati ambapo nchi ya Rwanda isipokua mshindi katika mashindano yoyote, hapo alidokezea mchezo ya mbio na kadhalika.

Alisema’’ baadhi ya hao wanaoshinda mashindano wana maisha kama ya sisi, wanaishi mazingira kama yetu, kuna mojawapo wanaoishi katika mazingira ya milima milefu kama sisi, si wala kwa upungufu wa wale wanaoipanda milima hiyo na kuiteremka bali kuna wengine wanaoipanda na kuiteremka wakibeba mizigo.

Rais Kagame alipata fursa ya kumpa hongera shujaa wa kike Salome Nyirarukundo, aliyewahi kushinda medali ya dhahabu kutoka Morocco mwezi uliopita. Aidha, alishtumu wizara ya michezo, ambayo haikuweza kumpa usaidizi wowote, hadi kushinda usiku kwenye viwanja vya ndege na bila chakula. Rais akaonya wahusikao na jambo hili.

bonyeza hapa kupokea gazeti juu ya facebook juu ya twitter

Richard Wa Billy

Izindi wakunda

Tanga Igitekerezo

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.

Bwiza.com