kwamamaza 7

Rais Kagame azindua matumizi ya Drone

0

Rais wa Rwanda Paul Kagame alianzisha kirasmi matumizi ya drone, ndege zisizokuwa na madereva zinazotumiwa katika huduma ya kupereka damu kwa hospitali tofauti nchini Rwanda. Kagame alitoa uzinduzi  katika sherehe ilifanyika jana wilayani ya Muhanga.

Matumizi ya ndege hizi huzuia kuchelewa kwa huduma za afya wakati wa kupewa damu nyingine kutoka hospitali moja na kuelekea nyingine.

Rais kagame alisema kwamba Rwanda imezoea kukaribisha ubunifu hasa hasa wakati unakuwa na lengo maalum ya kutatua changamoto za nchi.

30318707765_bd3a3e0132_z

“ninaamini kwamba mradi huu utahamasisha ubunifu zaidi na uwekaji wa mali katika biashara na mambo ya teknolojia nchini Rwanda. Tunataka kuharakisha na kuwapatia wananchi wa Rwanda mafunzo kwani teknolojia inakuwa muhimu wakati inawasaidia wananchi na kutatua changamoto katika shughuli mbali mbali”.

 

Keller Rinauo ambaye ni kiongozo na mwanzishi wa kiwanda kinachozalisha hizi drone, Zipline Inc. alisema kwamba maendeleo na utashi wa serikali yawezesha kukuza huduma hii kwa wananchi.

Keller alieleza kwamba baada ya kutengenezwa vizuri, mradi huu utawasaidia takribani milioni 6 za wananchi wanaohitaji msaada wa matibabu kwa udharura.

Théogène U @Bwiza.com

Leave A Reply

Your email address will not be published.

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.