kwamamaza 7

Rais Kagame awataka SADC kutatua suala la usalama nchini DR Congo

0

Rais wa Rwanda na Kiongozi wa Umoja wa Afrika (UA) amewataka washiriki wa Muungano wa SADC kutoa mchango wa kutatua masuala ya kisiasa na ya usalama nchini DR Congo.

Rais Kagame jana tarehe 17 Ogasti kwenye mkutano wa SADC nchini Namibia,Kagame amesema SADC inastahili pongezi kutokana na   mchango iliotoa kutatua masuala ya usalama nchi nyingine kama vile Madagascar Lesotho na kwingine.

“ SADC ilitoa mchango katika kutatua masuala ya usalama nchini Lesotho, Madagascar na Comoros na hivi karibuni nchini Zimbabwe. Kazi sawa nah ii inawasubuli nchini DR Congo” Kagame amesema

Rais Kagame amesisitiza jambo la usalama linastahili kutiwa kwenye msitari wa mbele kwa ujumla ili kulenga shabaha la UA.

Rais Kagame alitua nchini Namibia juzi kwa kuhudhuria mkutano wa SADC kwa mala yake ya 38 ambako marais na wakuu wa serikali watajadili namna ya kuwapa fursa vijana katika maendeleo na  kuboresha miundo mbinu.

Fred Masengesho Rugira/Bwiza.com

 

Leave A Reply

Your email address will not be published.

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.