Swahili
Home » Rais Kagame awakosoa mawaziri wasiozuru wakazi na kukaa ofosini zenye ‘Air Conditioner’ tu
HABARI MPYA

Rais Kagame awakosoa mawaziri wasiozuru wakazi na kukaa ofosini zenye ‘Air Conditioner’ tu

Rais Kagame amewakosoa mawaziri ambao wanakaa ofisini bila kuzuru wakazi kwa kujua mahitaji yao.

Rais Kagame  kwenye mkutano wa chama cha RPF-Inkotanyi jana tarehe 8 Julai 2018, amesema viongozi hawana budi kukaribiana na wakazi na  ili kujua changamoto wanazokabiliana nao mahitaji na  kuacha kuzuru mahali fulani wanapojua kuwa atakuenda huko.

“ Hamna budi kufanya utekelezaji wa wajibu wenu. Hamuezi  kufanya ufuatiliaji wa mambo kwa kukaa ofosini tu. Lazima kuenda kule kusiko na ‘Air Conditioning” ule upepo wa kijijini ni mwanana pia” Rais Kagame amesema

“ Nawaona ninapoenda huko kijijini, mnanifuata siyo kwa kazi bali kwenye ‘protocol’.Acha niwaambie, nawaonya sitaki wale ambao wananifuata. Muende huko wenyewe,mimi sitaki ‘protocol” ameongeza

Rais Kagame ameweka wazi kuwa maneno haya yatasisitizwa katika mkutano wa baraza la mawaziri na kuwakosoa wanaovaa viatu virefu wakati ambapo wamekuenda huko milimani.

” Nawaona hamuendi kufanya kazi”

Rais Kagame huwahasmasisha viongozi mala nyingi kujua hali ya wakazi kuhusu utekelezaji wa miradi mbalimbali ya serikali kama vile miundo mbinu.

Fred Masengesho Rugira/Bwiza.com

 

Izindi wakunda

Tanga Igitekerezo

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.

Bwiza.com