kwamamaza 7

Rais Kagame atoa msamaha, Wafungwa zaidi ya 800 waachiliwa huru

0

Wafungwa 870 kwa ujumla wameachiliwa huru leo 15 Disemba 2016 kulingana na msamaha wa rais Kagame uliotolewa katika maamuzi ya kikao cha baraza la mawaziri wiki iliyopita, na wengine wameachiwa kulingana na amri ya waziri wa sheria.

Miongoni mwa hawa 870, kuna watoto walihukumiwa pamoja na wanawake walihukumiwa kwa dhambi ya kutoa mimba 62 ambao walisamehewa na rais Paul Kagame. wengine 808 wameachiliwa kulingana na amri ya waziri wa sheria ya tarehe 14 Ukuboza 2016.

[ad id=”72″]

Msemaji wa taasisi ya kuwachunga wafungwa na wanaokosolewa, CIP Sengabo Hillary alisema kwamba isipokuwa wanawake walitoa mimba na watoto, miongoni mwa walioachiliwa huru hawakuwemo walioshiriki katika mauaji ya kimbari.

abagore

“Walioachiliwa huru ni wale walifanya dhambi za kawaida isipokuwa mauaji ya kimbari, dhambi za rushwa na wasaliti wote kutoka katika gereza 14.” CIP Sengabo aliongeza kwamba walioachiwa huru ni wale walionyesha tabia nzuri na kuomba msamaha.

Wafungwa hawa ambao wamesamehewa, wamelazimishwa kuwa na tabia nzuri katika jamii na kuepukana na dhambi tena ili wasirudishwe gerezani.

bonyeza hapa kupokea gazeti juu ya facebook juu ya twitter

@Bwiza.com

Leave A Reply

Your email address will not be published.

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.