kwamamaza 7

Rais Kagame atoa matumaini kuhusu ubalozi wa Ufaransa nchini Rwanda

0

Rais Kagame ametangaza inawezekana kuwepo ubalozi wa Ufaransa nchini Rwanda kulingana na ushrikiano ulioko kati ya nchi mbili.

Rais Kagame ametangaza haya alipokuwa katika mazungumzo na  Jaune Afrique.

Rais Kagame alisema jambo muhimu ni kwamba hata kama jambo hili haiwezi  kutekelezwa kwa muda mfupi cha muhimu ni  kwamba ushirikiano kati ya Rwanda na Ufaransa una mwelekeo mzuri.

Kwa kujibu mtangazaji Francosi Soudan alisema” Kama nilivyoeleza haya mambo yana uhusiano, je,hili ni jambo la kutekelewa wiki au mwezi? Tutafanya uchunguzi, Jambo la msingi ni kwamba kuna mwelekeo mzuri”

Rais Kagame amesema haya baada ya Kiongozi wa Ufaransa kwa mambo ya nje nchini Rwanda,Etienne de Souza.

“Tunajaribu kutumia fursa yoyote tunayo,kulikuwepo wakati ambapo nchi hizi mbili zilipata fursa.Nafikiri kuwa tungali njiani ya kubadili mambo” de Souza alisema

Pia, Mwandishi Jean-François Dupaquier, alimuandikia Rais Macron kwa kumkumbusha  huu ni wakati wa kuboresha ushirikiano kati ya  Rwanda na Ufaransa.

“Namna gani Paris inaweza kushirikiana na Kigali? Cha muhimu ni ukweli.Kunahitajika uchunguzi wa maandishi ya ikulu kati ya mwaka 1990-19 “Kutimiza hili kitakuwa kitendo cha Rais Macron kutekeleza aliyoahidi Ufaransa” Dpaquier aliongeza.94”aliandika

Ufaransa hauna ubalozi nchini Rwanda tangu mwaka 2015  baada ya Michel Flesch kumaliza mamlaka yake.

Ushirikiano kati ya Rwanda na Ufaransa ulianza kuwa mkia wa mbuzi tangu mwaka 1994 ambako Rwanda ilishtaki Ufaransa kushiriki katika mauaji ya kimbali dhidi ya Tutsi. Hata hivyo, Ufaransa ulikanusha haya mashtaka yote.

Fred Masengesho Rugira/Bwiza.com

 

 

 

 

Leave A Reply

Your email address will not be published.

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.