kwamamaza 7

Rais kagame apewa tuzo ya kuboresha elimu ya sayansi

0

Rais wa jamhuri ya Rwanda Paul Kagame amepatiwa tuzo katika uzinduzi wa mkutano kimataifa wa 27 kuhusu kuendeleza sayansi. Tuzo hio amepatiwa leo 14 Novemba 2016, ametunukiwa kwa ajili ya kurekebisha elimu ya sayansi na teknolojia.

Mkutano wa chuo cha sayansi, TWAS (The World Academy of Sciences) umeanza leo na utaisha Alhamis, 17 Novemba 2016; umeshirikiwa na wataalam kutoka nchi 52.

Kagame amewashukuru waliomtunukia tuzo na kusema kwamba ni ya wanyarwanya wote kwa ajili ya kutia bidii kwa kujenga nchi. “Tuzo tumepewa ni ya wanyarwanda wote walifanya juu chini ili kujenga nchi. Tangu zamani watu walitumia sayansi ili kufikia majibu ya swali wanakuwa nazo.”

[ad id=”72″]

Wengine walipewa zawadi na TWAS kutokana na mchango wao katika utafiti wa sayansi ni Samira Omar kutoka Kuwait, Prof frank kutoka Uingeleza na Prof Jean Bosco Gahutu aliyefanya utafiti kuhusu mchango wa maharagwe kwa kuongeza damu mwilini.

TWAS iliundwa na kundi la wahenga katika sayansi mnamo mwaka wa 1983. Wahenga hao walikuwa na wazo kuu la kurekebisha elimu ya sayansi na kusaidia nchi zinazojirekebisha kimaendeleo.

bonyeza hapa kupokea gazeti juu ya facebook juu ya twitter

Theogene U @Bwiza.com

Leave A Reply

Your email address will not be published.

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.