kwamamaza 7

Rais kagame ajiunga na raia wa Kicukiro kwenye “Umuganda”

0

Rais Kagame amejiunga pamoja  na raia wa Kicukiro katika shughuli ya Umuganda iliyofanyika jumamosi ya tarehe 24 Juni 2015 katika sehemu ya ardhi oevu ya Nyandungu iliyotengwa kwa ajili ya utalii.

Shughuli hiyo ya umuganda imejumuisha na vitendo vya kupanda miti ya minazi. Hapo rais wa Jamhuri ya Rwanda alisema kwamba amefurahishwa na kushirikiana na raia katika shughuli hii.

“Haifai kuchukuwa kiholela umuhimu wa Umuganda kwa sababu unaashiria ushirikiano , ndoto na bidii ya pamoja. Nawashkuru sana kwa kushiriki katika shughuli hii ya Umuganda. Ninyi wote vijana, wasichana, wavulana na wazee endeleeni kuwa na ushirikiano wa pamoja, endeleeni kuwa na mawazo ya kujijenga na kuijenga pia nchi ili tuifanye kuwa na maendeleo na usalama unaostahili. Mnyarwanda aishi kwa usalama na ajiendeleze” rais amesema

Akigusia umuhimu wa kutunza ardhi oevu amesema kwamba ni mazingira yanoyostahili kutunzwa. Kwa hiyo ametoa wito kwa wale ambao wangali wanaendesha shughuli zao katika maeneo kama hayo nchi kote kuzihamisha.

“Wanaodendesha shughuli zao katika maeneo ya ardhi oevu zikiwa hakupangiwa kuendeshwa hapo wanapaswa kuzihamisha na kuacha mahali hapo kutunzwa. Tutalitolea suluhu tatizo hili, hapa wamiliki wa shule, wale waliojenga hifadhi za mifugo na watu wengine wanaopaendesha shughuli ambazo haziruhusiwi kuendeshwa kwa maeno kama haya ndio wanaonywa” rais asema

Ameendelea kusema kwamba kuna wale waliovamia ardhi kama hiyi na kupajenga kwa shughuli za kibinafsi ambazo ni kinyume na sheria wakijitetea kwa kuwa wana ruhusa kutoka kwa viongozi, lakini hao wote pia ni wa kulaumiwa.

Serikali imewasidia watu kuhamisha shughuli zilizokuwa zikiendeshwa katika maeneo kama haya  na hata kuwahimiza kusitisha wale ambao wangali wanaendesha shughuli zao katika maeneo kama hayo.

Serikali iliweka mikatakati na kanuni mbalimbali kwa ajili ya kuhifadhi na kutunza mazingira ya ardhi oevu. Ardhi oevu ya Rugezi ilitunzwa kulingana na utaratibu huo hadi liingie katika maeneo yenye unyevu na ambalo ni muhimu kwa kiwango cha kimataifa( (Wetlands of International Importance).

Kwa hiyi Rwanda inaendelea kuzishughulikia ardhi oevu nyingine na kuitunza ili iweze kufika kwa kiwango kama hicho.

Kulingana na takwimu kutoka REMA za mwaka wa 2008 Ofisi ya Nchi ya Kutunza Mazingira maeneo kama haya yanachukua nafasi ya 10.6% ya ardhi ya Rwanda na jumla ya ardhi oevu  860.

Ardhi hii ya Nyandungu ambapo umuganda ulifanyika ina upana wa hekta 134. Mahali hapa pataandaliwa kuwa kivutio cha utalii na hii ni kwa kipindi cha miaka mitano, mradi huu unatarajiwa kugharimu bilioni 2 za faranga za Rwanda.

bonyeza hapa kupokea gazeti juu ya facebook juu ya twitter

 Richard Wa Billy

Leave A Reply

Your email address will not be published.

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.