Home HABARI MPYA Rais Kagame ajiuliza ka nini ufukara unajitokeza barani Afrika miaka nenda rudi
HABARI MPYA - June 23, 2018

Rais Kagame ajiuliza ka nini ufukara unajitokeza barani Afrika miaka nenda rudi

Rais Kagame kwenye mkutano wa ‘ Africa Transform 2018’ nchini Ghana,  amesema haelewi namna ambavyo ufukara unakumba bara la Afrika miaka nenda rudi kinyume na kuwa kuna mali ya kutosha.

Katika hotuba yake Rais Kagame ameeleza mali ya Afrika ina uwezo wa kusaidia utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo kwa wakazi na kuwa haya yatawezekana kwa matumizi bora ya mali ya Afrika.

“Ukizungumza mabadiliko inastahili kuwahusisha wakazi na mali tuliyonayo  ambayo inastahili matumizi bora. Tunazungumza kuhusu matumizi bora ya mali na siasa nzuri zitakazotusaidia kufika tutakapo” Kagame amesema

Hatuna maelezo namna ambavyo ufukura unajitokeza miaka nenda rudi tukiwa na mali asili hii” Kagame amesisitiza

Kwenye huu mkutano wamealikwa waheshimiwa wengine wakiwemo Rais Nana Akufo-Ado wa Ghana, Makamu Rais wa Ghana , Mahamudu Bawumia,  Makamu Rais wa Cote d’Ivoire, Daniel Kablan Duncan, tajiri wa kwanza barani Afrika, Aliko Dangote na Waziri wa Mali nchini Rwanda Dk. Uzziel Ndagijimana na wengine.

Huu mkutano unalenga kuhojiana namna za kuanda kazi,kuboresha uwekezaji na kuanzisha siasa za kubadili mfumo w mambo barani Afrika.

Fred Masengesho Rugira/Bwiza.com

 

 

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.