kwamamaza 7

Rais Kagame ajibu mawaziri Busingye na Nduhungirehe kuhusu wanawake wanaovaa nguo fupi hadharani

0

Rais Kagame amejibu waziri wa haki, Johnston Busingye na waziri makamu kwenye wizara ya mambo ya nje,Olivier Nduhungirehe kuhusu wanawake wanaovaa nguo fupi hadharani.

Waziri Busingye alikuwa akipinga hizi tabia kwa kusema “Hizi mantiki zisizo na umuhimu hazihitajiki” na mwenzake Olivier Nduhungirehe alikuwa akitetea kwa kusema” Tatizo ni yule mwanamume anayeangalia huyo mwanamke anayevaa nguo fupi,siyo huyo mwanamke.Tuache hizi fikra zisizoeleweka” .

Kwenye mkutano wa EDD 18 nchini Ubelgiji, Rais Kagame amesema wanawake wanapaswa  kujali wanavyoonekana hadharani na hata kwa kitone cha sauti zao.

“ Haitoshi kuwa wanawake ni wazuri kama wenzao wa jinsia ya kiume. Wanahitaji pia kuwa wanyenyekevu wanavyoonekana hadharani na kwa kitone cha sauti lao(…)”

Pengine, Rais Kagame  amezungumzia kuhusu unyanyasaji unaofanyiwa wanawake kwa kusema ni tabia inayostahili kupigwa marufuku.

“Tabia ya kuwanyanyasa wanawake ni kodi kubwa kwa haki zao(…) Haina budi kupigwa marufuku” Rais Kagame amesema

Rais Kagame amefunguka haya baada ya migogoro kuzuka kwenye  twitter nchini Rwanda watu wakisema kwamba wanawake wananyanyaswa kuhusu wanavyovaa .

Fred Masengesho Rugira/Bwiza.com

Leave A Reply

Your email address will not be published.

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.