Home HABARI MPYA Rais Kagame afunguka RDF huwamalizia kazi wanaoleta vita
HABARI MPYA - July 13, 2018

Rais Kagame afunguka RDF huwamalizia kazi wanaoleta vita

Rais Kagame amesema RDF hufunzwa kupambana katika vita na siyo kuanzisha vita ila huwa tayali kuwamalizia kazi wanaoleta vita kwake.

Rais Kagame amesema haya leo tarehe 13 Julai kwenye sherehe ya kuapisha rasmi maafisa wadogo 180  wanaomaliza mafunzo ya kijeshi.

Rais Kagame amesema” RDF wanafundishwa na ni tayari  kupambana katika vita lakini siyo kuanzisha vita kwa watu wengine. Wengine wanapozusha vita hapo tunatumia  fikra na jitihada na tuka wamalizia hili suala” Kagame amesema

Pia Kagame amewataka hawa maafisa kufanya liwezekanalo kulinda Wananchi.

“Mlipata ujuzi wa kupambana na vita,kulinda nchi na Wanyarwanda. Ni kazi umuhimu sana, nawashukuru wote waliomaliza masomo yao,ni tukio la kujivunia” ameongeza.

Maaafisa 180 wenye cheo cha Sekendi Luteni wamemaliza masomo yao kwenye Shule la Jeshi la Gako, mashariki mwa Rwanda.

Fred Masengesho Rugira/Bwiza.com

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.