kwamamaza 7

Rais Kagame afunguka kwa nini alifanya jaribio la DNA

0

Rais Paul Kagame amefichua sababu iliyomfanya afanye jaribio la Deoxyribonucleic Acid (DNA) hata kama anaona ni taarifa zinazostahili kuwa siri.

Rais Kagame ametangaza kuhusu hili jaribio alipokuwa katika  mazungumzo na Jaune Afrique wiki iliyopita.

Huyu kiongozi alimuambia mtangazaji  Francois Soudan kuwa alifanya majaribio ya DNA kwa sababu ya udadisi wa kisayansi.

“ Ingestahili kuwa siri,lakini, acha nikuambie. Ni kwa ajili ya udadisi mdogo wa kisayansi” Kagame alisema

“ Hakuna jambo jingine juu ya hayo” aliongeza

Akijibu kuhusu matokeo la jaribio , Rais Kagame alisema kuwa yalikuwa mchanganyiko wa kiasili.

“ Mchanganyiko wa kiasili: African, European,Asian,Tutsi,Hutu…

Nami ni mwanadamu anayewaona watu wengine kama viumbe bila kujali kama kuna wale wanaoamini watu waliumbwa au ni mabadiliko. Huyo ndiye mimi” Kagame alisisitiza

Rais Kagame ni mmoja mwa watu ambao ni nadra kusema kuhusu mambo yao  binafsi hadharani.

Fred Masengesho Rugira/Bwiza.com

 

Leave A Reply

Your email address will not be published.

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.