kwamamaza 7

Rais Kagame afunguka kuhusu masuala ya Jen.Kayumba Nyamwasa na Faustin Twagiramungu

0

Rais Kagame amesema kwamba serikali ya Rwanda haikumuzuia  Twagiramungu Faustin kurejea nchini na kuwa si vizuri  serikali ya Afrika Kusini kuhudumia mtu anayetaka kushambulia nchi yake.

Kwenye mazungumzo na Jaune Afrique, Rais Kagame ameeleza Faustin Twagiramungu anaweza kuomba ‘Visa’ akiwa nchini Rwanda.

“ Twagiramungu anataka Passport ya kuenda wapi? Ana uraia wa Ubelgiji,naona anapenda kuishi huko. Hataki passport ya Rwanda kuja hapa. Passport yake atayipata huko Kigali. Hii ndiyo hali”

Nambari 2996 ya hiki chombo cha habari na mtangazaji Francois Soudain, Rais Kagame alisema jambo la Jen. Kayumba Faustin Nyamwasa kuishi nchini Afrika Kusini litajadiliwa.

“Nafikiri kwamba siyo vizuri nchi kuhudumia mtu anayelenga kushambulia nchi asili yake. Kwa hiyo, tutaendelea  kuwasiliana na Afrika Kusini kuhusu hili jambo lakini siyo sababu ya kuboresha ushirikiano wetu”

Jen. Kayumba Faustin  Nyamwasa alikimbilia nchini Afrika Kusini mwaka 2010 na kuunda chama ‘Rwanda National Congress’.

Mwanasiasa Faustin Twagiramungu alijiuzuru kwenye nafasi ya Waziri Mkuu mwaka 1995 na kukimbilia nchini Ubelgiji na kuunda chama RDI-Rwanda Rwiza.

Huyu alisikika mala nyingi akitangazakuwa serikali ya Rwanda ilimzuia kurejea nchini Rwanda.

Fred Masengesho Rugira/Bwiza.com

 

 

Leave A Reply

Your email address will not be published.

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.