kwamamaza 7

Rais Kagame afungua rasmi shughuli za ujenzi wa Kiwanja cha Ndege cha Bugesera

0

Siku ya leo tarehe 09 Agosti kumefanyika hafla za kufungua rasmi shughuli za ujenzi wa kiwanja cha ndege cha Kimataifa cha Bugesera. Shughuli hiyo ilikiwa ikiongozwa na rais Kagame ambaye amesema kiwanja hiki kitasaidia kuinua uchumi wa nchi.

Rais Kagame ambaye ameweka jiwe la msingi kama ishara ya kufungua rasmi shughuli za ujenzi za Kiwanja hicho alipohotubu alibainisha kwamba kiwanja hicho  hakinatarajiwi tu kuwanufaisha wanyarwanda bali na waafrika wengine hasahasa kwa kibiashara na uwekezaji.

[xyz-ihs snippet=”google”]

“Kiwanja cha Ndenge cha Bugesera kitasaidia kuinua uchumu wa Rwanda na hata ushirikiano wa kibiashara wa eneo hili” Kagame amesema.

Rais Kagame alihimiza ushirikiano wa wadau wote ili kuweza kumaliza shughuli za ujenzi wa kiwanja hiki kwa muda. “huyu ni mradi ambao tumekuwa tukiungoja kwa kipindi kirefu na nina imani sisi wote tutashirikiana ili shughuli hizi ziweze kumalizika kwa muda na kiwanja kiweze kutumiwa”

Hapa rais Kagame aliahidi kwamba shughuli za ujenzi wa kiwanja hiki zitamalizika mnamo siku za hivi karibuni na kuna imani watakuwa hapa baada ya si mrefu kwa hafla ya uzinduzi wa shughuli za kiwanja.

Kiwanja hiki kinatarajiwa kumalizika kwa gharama ya milioni 418 za dola za kimarekani na zinatarajiwa kukamilika mnamo mwishoni mwaka wa 2018 na kitakuwa na uwezo wa kupokea abiria milioni 4.5 kwa mwaka.

Bonyeza hapa kupata habari za hivi karibuni kwenye facebook na twitter

Richard Wa Billy

Leave A Reply

Your email address will not be published.

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.