Home HABARI MPYA Rais Edgar Lungu kutua Rwanda,vyombo vya habari vyafunguka lengo lake
HABARI MPYA - February 21, 2018

Rais Edgar Lungu kutua Rwanda,vyombo vya habari vyafunguka lengo lake

Ikulu ya Zambia kupitia afisa wa mawasiliano,Amos Chanda imeweka wazi  kwamba Rais  Edgar Chagwa Lungu anatarajia kutua nchini Rwanda kwenye ziara ya kikazi ya siku mbili.Hata hivyo,vyombo vya habari mbalimbali vimeanza kukosoa ziara hii kwa kuweka wazi lengo la ziara hii.

Chombo cha habari kwa jina la Zambiawatchdog.com kimetangaza kuwa Edgar Lungu amekuja nchini Rwanda kumuomba ushauri wa Rais Kagame kuhusu namna ambavyo anaweza kuendelea kukaa madarakani.

Kimeandika”Amekataliwa kufanya safari za kimataifa kwa sasa ameelekea Rwanda,Ni kumuuliza Rais Kagame anavyoweza kufanya kwa kuendelea kutawala nchi”.

Hiki chombo cha habari kimeendelea kusema kwamba Rais Lungu anaweza kuja akaenda kule nchini Burundi kumkuta Rais Nkirunziza kuhusu hili suala.Pengine hili limehusishwa na ziara ya Rais wa DR Congo,Joseph Kabila nchini Zambia.

[xyz-ihs snippet=”google”]

Kinyume na hili  inatarajika kuwa huyu rais anakuja nchini Rwanda kuhojiana namna ambavyo Rwanda ilipiga hatua ya maendeleo kiuchumi kwa uongozi wa Rais Paul Kagame.

Rais Edgar Lungu alikaa madarakani tangu Januari mwaka 2015.Wapinzani wake walimbatiza “tourist Edgar Lungu” yaani mtalii Edgar Lungu juu ya safari zake za kila mala ugenini.

Subscribe to BWIZA TV to get news and song updates

Bonyeza hapa kupata habari za hivi karibuni kwenye facebook na twitter

Fred Masengesho Rugira/Bwiza.com

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.