kwamamaza 7

Raia wa Wingereza kuwa mfalme wa Rwanda baada ya miaka 64

0

Baada ya kifo cha mfalme wa Rwanda, Kigeli V Ndahindurwa, wakalimani wamemtaja Bushayija kumkomboa. Raia wa Uingeleza walifurahia habari hiyi, kuwa ndugu yao Bushayija anakuwa mfalme, baada ya miaka 64, wakati wa mfalme George VI.

Magazeti ya Telegraph, The Times, The Guardian, na The Sun, yalikuwa ya kwanza kumpongeza, huyu aliyekuwa mtumishi wa Pepsi Cola nchini humo. Habari hii ya furaha, hufuatana na ya kuhusu Gambia, napo raia wa Wingereza amechaguliwa kuwa rais, Adama Barrow.

[xyz-ihs snippet=”google-pub”]

Bushayija Emmanuel, anaye kamata na fasi ya mfalme marehemu Kigeli V Ndahindurwa, ni baba wa watoto wawili. Anaishi Uingeleza, Old Trafford na familia yake, kutoka mwaka 2000. Alizaliwa Rwanda, akaishi Uganda kama mkimbizi, akarudi nchini mwake, baadaye ndipo aliamuwa kwenda kuishi Ulaya.

Tarehe 9 Januari mwaka huu, ndipo msemaji wa mfalme Kigeli, Boniface Benzige, ametangaza Bushayija kama mfalme mpya wa Rwanda, atakayeyitwa Yuhi VI. Benzige amesema, toka 2006 marehemu  Kigeli  Ndahindurwa  pekee, ndiye amemchagua Bushayija kuwa mfalme.

[xyz-ihs snippet=”google-pub”]

Hatimaye Mfalme mpya Bushayija haja tangaza kitu kuhusu hizi habari za ufalme wake, na bali hazikutangazwa siku ya mazishi ya Kigeli, aliyofanyiwa jana tarehe 15 January, kijijini Mwima, wilaya ya Nyanza, mkoa wa kusini. Mmoja mwa nduguze, aliambia The Guardian kama Bushayija hataki kuongea na watangazaji habari.

Nchini Rwanda, ufalme wa Bushayija haujulikane kamwe, wala haukubaliwe hata. Pasta Ezra Mpyisi, aliyekuwa mshauri wa mfalme Kigeli wakati akiongoza Rwanda, amesema ufalme wa Bushayija hautajulikana, kwani  ulitangazwa na Benzige, mkalimani wake; si nduguye, wala hana uhusiyano na ufalme wa Rwanda.

Kutoka 1961, Rwanda ilifukuza ufalme ikaingiza uongozi wa kijamhuri. Referandumu imeonyesha kwamba wanyarwanda asilimia 80 hawakubali ufalme, ingawaje marehemu Kigeli hakuitika izi hesabu.

bonyeza hapa kupokea gazeti juu ya facebook juu ya twitter

[xyz-ihs snippet=”google-pub”]

JB Karegeya@bwiza.com

Leave A Reply

Your email address will not be published.

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.