kwamamaza 7

Raia wa Rwanda Evariste Munyensanga akosekana Marekani

0

Polisi ya mji wa Portland huko Marekani imeanza kumtafuta Munyensanga Evariste, raia wa Rwanda aliyekosekana tarehe 18 Novemba 2016.

Munyensanga mwenye umri wa miaka 29, alizaliwa wilayani Kamonyi na alielekea Marekani takribani miezi 5 iliyopita.

Ndugu zake wanaoishi pamoja Marekani, mjini Portland amesema kwamba Evariste alibebwa garini na mtu asiyejurikana ; tangu alipokosekana na mitandao yake ya kijamii haitumishwi tena.

Nibayahore Ancille ambaye ni mamake anayeishi wilayani Kamonyi, alithibitisha habari na kuambia Bwiza.com kwamba wiki mbili zimepita bila maongezi ya simu na mvulana wake na hivi wiki moja na nusu imepita tangu alipata habari za kukosekana kwake.

nsanga3
Munyensanga Evariste wa kati mwenye mpira wa kijani

“Tumepigiwa simu na ndugu wake walikuwa wanaishi pamoja, walituambia kwamba amekosekana wiki moja na nusu iliyopita. Tutaendelea kuuliza, labda ataonekana.” Mama yake Ancille Nibayahore alisema.

[ad id=”72″]

Munyensanga Evariste ambaye alikuwa mwanafunzi wa chuo kikuu, mnamo 2011 ndipo aliumizwa na ugonjwa wa moyo hadi alipofanyiwa upasuliaji na timu ya waganga katika shirika la Healing Hearts Northwest for heart surgery for heart surgery; baadaye akaelekea Marekani.

Balozi wa Rwanda nchini Marekani Bi Mathilde Mukantabana alisema kupitia kwa ukurasa wake wa Twitter kwamba kesi ya kukosekana kwake inafuatiliwa na polisi ya Maine mjini Portland.

bonyeza hapa kupokea gazeti juu ya facebook juu ya twitter 

Theogene U @Bwiza.com

Leave A Reply

Your email address will not be published.

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.