Swahili
Home » Raia wa Rwanda auawa nchini Uganda
HABARI MPYA

Raia wa Rwanda auawa nchini Uganda

Polisi ya Uganda imewakamata watu wanne wanaotuhumiwa kuhusika na kifo cha Mnyarwanda, Tuzabana, 20, aliyekuwa mkazi kijijini Bakijulula wilayani Mityana.

Kuna taarifa kwamba malehemu ameuawa na kundi la watu baada ya kujaribu kumbaka mwanamke kwa jina la Frolence ambaye ni mwenyeji wa hoteli kijini humo.

[xyz-ihs snippet=”google”]

Inasemekana kuwa mwanamke huyu alishiriki katika kitendo cha kumpiga Tuzabana hadi alipofariki.

Mwili wa malehemu umepelekwa hospitali ya Mityana ili kufanyiwa uchunguzi wa chanzo cha kifo hiki.

Kwa mujibu wa taarifa za The Spy Reports,Tuzabana alikuwa mfanyakazi wa kawaida wa kampuni ya kiwanda cha chai Tameko.

Bonyeza hapa kupata habari za hivi karibuni kwenye facebook na twitter

Fred Masengesho Rugira/Bwiza.com

Izindi wakunda

Tanga Igitekerezo

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.

Bwiza.com