Swahili
HABARI

Raia wa Rwanda 90 wafukuzwa nchini Uganda.

Maafisa wa bodi ya Uhamiaji nchini Uganda jana wamefukuza raia wa Rwanda 90 ambao waliingia nchini Uganda kinyume na sheria.Jambo hili limekamilika kwa msada wa kikosi cha polisi na wanajeshi cha Makenke mjini Mbarara na kuwarudisha kwao  kwa kutumia magari mawili makubwa usiku uliopita.

Magari yakijianda kurudisha Raia wa Rwanda kwao.

Kiongozi wa Ofisi ya Upererezi ya kikosi cha pili cha Makenke,Fred Mushambo amesema kuwa Raia wengi wa Rwanda wanaishi nchini Uganda kinyume na sheria watarudi kwao kwa kuwa kitendo hiki kitaendelea na kukumbusha wengi kuwa Uganda siyo mahali pa kuishi kwa namna watu watakayo.

Kiongozi huyu amendelea akisema kwamba viongozi wa usalama wameisha jianda vilivyo kupamabana na tatizo hili la kuwa Wanyarwanda wengi wanaishi nchini Uganda bila vitambulisho na pia wanafanya makosa mengi ya uharibu na kuwa hawana sababu muhimu ya kuenda nchini Uganda kama inavyotangazwa na Chimpreports.

Kwa upande mwingine,Watangazaji walikatazwa kufuata jambo hili lilipofika kwenye hatua ya Wanyarwanda waliokamatwa kurudishwa kwao kwa kuwa limefanyika majira ya usiku wa manane.

Maafisa wa bodi ya Uhamiaji nchini Uganda jana wamefukuza raia wa Rwanda 90 ambao waliingia nchini Uganda kinyume na sheria.Jambo hili limekamilika kwa msada wa kikosi cha polisi na wanajeshi cha Makenke mjini Mbarara na kuwarudisha kwao  kwa kutumia magari mawili makubwa usiku uliopita.

Bonyeza hapa kupata habari za hivi karibuni kwenye facebook na twitter

Fred Masengesho Rugira/Bwiza.com

Izindi wakunda

Tanga Igitekerezo

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.

Bwiza.com