kwamamaza 7

Raia wa Ngoma wakabiliwa na ukosaji makazi bada ya nyumba zao kubomelewa na serikali

0

Imekuwa siku ya tatu Viongozi wa ngazi za chini pamoja na vikosi vya walinda usalama wilayani Ngoma wakiendelea na shughuli ya kubomoa nyumba za raia wanaodiawa kujenga kinyume na sheria. Ingawa nyumba za raia hao zinabolewa wao wasema kwamba walizijenga nyumba hizo viongozi wakiwa wanafamu.

Baadhi ya raia ambao walihojiwa na tovuti yetu bwiza.com, wamesema kuwa huenda wakabomolewa makazi yao wakati zilijengwa kwa ruhusa kutoka  ya baadhi ya viongozi wa ngazi za chini na hakuna sababu kubomolewa nyumba kwani zilijengwa viongozi hao wakiwa wanafahamu.

[xyz-ihs snippet=”google”]

Bi. Nyirabasangwa Claudine ambaye ni mkazi wa Remera, amesema kuwa kabla kujenga nyumba yake uongozi ndio ulimsaidia kupata msaada wa mabati na uinuaji wa nyumba, kwani nyumba yake ilikuwa imeharibiwa na mvua, kwa hiyo hawana haja ya kumfutia makao.

Amesema: “viongozi wa tarafa wamenisaidia kupata mabati na fundi wa kujengea, nyumba imemalizika na hivi wako wanaibomoa, najiuliza kwa nini badala ya kunibomolea nyumba hawakunizuia kabla ya kutumia mali yangu yote.”

Hakorimana Jean Claude ambaye ni mwenyeji wa kijiji cha Amarembo kata ya Cyasemarembo, Tarafani Kibungo naye amesema: “ nyumba yangu ambayo imebomolewa nimeishi nayo miaka 10 na nina vitambulisho kutoka serikali vya kuishi hapa na tena sikujua ni kinyume na sheria, ubomoaji wa nyumba yangu ni dhuluma ya haki ya binadamu kwani hawakutujulisha kwamba siyo mahali ya kuishi, hivi tunaelekea wapi?”

Raia hawa wanaangaika kwani hawana pengine pa kuelekea baada ya kufutiwa makazi, cha kuumiza tena ni kwamba baadhi yao waombwa pesa za kulipia wenye kubomoa nyumba hizo.

Mapendo Gibert, katibu mtendaji wa tarafa ya Kibungo, ameeleza kuwa shughuli hii na lengo ya kuboresha mji na mahali karibu nao na kuujenga kwa kisasa.

Anaendelea kusisitiza kwamba raia hawa wamekiuka sheria na kujenga nyumba mahali wasiporuhusiwa.

Amesema: “nyumba zilizobomolewa ni za watu ambao wamekiuka sheria ya makazi waliotolewa.”

 

nyumba zilizobomolewa

 

Bonyeza hapa kupata habari za hivi karibuni kwenye facebook na twitter

Richard Wa Billy

Leave A Reply

Your email address will not be published.

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.