kwamamaza 7

Raia wa Kayonza na ujanja mpya wa kuuza ng’ombe waliopewa kama msaada kupitia Girinka

0

Mojawapo wa raia wa tarafa ya Ramira ya Kayonza wawashtumu wenzake kuwauza ng’ombe walizopewa kupitia mfomo wa girinka Munyarwanda na wakadanganya kwamba wameibwa

“Hapa sehemu ya Nkamba ng’ombe huuzwa na nasikia sehemu nyingine ya Bugambira hali ni ile ile, lakini haifai kuwauza ng’ombe ambao raia walipewa kama msaada na kusiwe na hatua yoyote kufuatilia hili. Serikali yawataka raia kufuga na kujiendeleza ingawa mojawapo wanatumia mfumo huu kijanja kwa kujitafutia fedha” asema raia

Raia mwingine alisema kwamba wanasikitika kutopewa ng’ombe hawa na wakapewa wale ambao hawazitaki sababu inayowafanya kuwauza.

“Kuna raia mojawapo wanaopewa ng’ombe na badala yake wakawauza, hapa sehemu ya Nkamba kuna ng’ombe 4 waliouzwa siku za hivi karibuni, huenda wakapewa bila kuhitaji na tukanyimwa sisi ambao tunahitaji kupewa, wanao uadifa wa kutoa ng’ombe hao wangefanya uchunguzi kabla ya kuamua nani apewe” asema raia huyu

[xyz-ihs snippet=”google”]

Hata hivyo, uongozi wa wilaya unasema kwamba hauna habari kuhusu jambo hili kama inavyothibitishwa na meya wa wilaya ya Kayonza, Jean Claude Murenzi lakini aliahidi kwamba wanakwenda kulifuatilia jambo hilo.

“hatuna habari kuhusu kuwepo kwa suala la ng’ombe kuuzwa lakini tukiona kuepo kwake sheria zitatendwa” Meya asema

Ingawa uongozi wa wilaya unakana kuwepo kwa tatizo hilo, Gavana wa Jimbo la Mashariki, Judith Kanzayire alitoa kauli ya kuwaonya viongozi wasiofuatilia hali ya ng’ombe waliotolewaa kwa ajili ya Girinka na kuwafanya kutotunzwa ipasavyo. Kauli hii ilitolewa na Gavana katika sherehe za kumaliza wiki kwa ajili ya Girinka tarehe 5 Aprili 2017

Mfumo huu wa “Girinka Munyarwandwa” ulianza mwaka 2008 kufuatia wazo la rais Paul Kagame ukiwa na lengo la kuwatoa katika na umaskini raia wasiojiweza. Mfumo huu hivi sasa umewafikia takriban raia 87,228 wa jimbo la Mashariki, na inatarajiwa kwamba kutatolewa ng’ombe 101,179 kabla ya mwaka huu kuisha.

bonyeza hapa kupokea gazeti juu ya facebook juu ya twitter

 Richard Wa Billy

 

Leave A Reply

Your email address will not be published.

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.