Swahili
HABARI

Raia wa Gatsibo waathiriwa na kutumia maji machafu

Raia wa wilaya ya Gatsibo katika kata ya Gasange wanalalamika kwa ajili ya kukosa maji safi ya kutumia katika maisha ya kila siku, na hivi husababisha ugonjwa mbali mbali kama huthibitishwa na waganga wanaowahudumia raia.

Tatizo la kukosa maji huwasababisha raia kufanya safari ndefu ili kuweza kushota maji bondeni na pengine hutumia maji ya mvua ambayo hayana usafi wa kutosha.

Raia mmoja alisema, “Hatuna maji safi katani popote. Siku moja tunatumia maji kutoka bondeni, wakati mwingine tunatumia maji ya mvua.”

[xyz-ihs snippet=”google-pub”]

Matokeo ya kukosa maji safi yanathibitishwa na waganga kutoka kituo cha afya cha Gasange, husema kwamba idadi kubwa ya wagonjwa ni waathirika wa ugonjwa unaosababishwa na uchafu ; kama ilithibitishwa na mmoja miongoni mwao Matabaro Theophile.

Kiongozi makamu wa wilaya ya Gatsibo anayehusika na uchumi, Manzi Theogene alisema kwamba tatizo la ukosefu wa maji safi limejurikana lakini hakuna bajeti kamili ya kuridhisha miradi yote ya kuwanufaisha raia kama kujenga bilula kamili.

bonyeza hapa kupokea gazeti juu ya facebook juu ya twitter

@Bwiza.com

Izindi wakunda

Tanga Igitekerezo

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.

Bwiza.com