kwamamaza 7

Polisi yarejesha vifaa vya kujenga barabara vilivyoibwa

0

Tarehe 30 Oktoba 2016, polisi ya Rwanda imekamata vyuma tofauti ndani ya gari katika wilaya ya Karongi vilivyoibwa kampuni ya uchina “China Road and Bridge Corporation” ambayo hujenga barabara katika wilaya ya Rusizi, Karongi na Rubavu.

Msemaji wa polisi mkoani magharibi Chief Inspector of police Theobald Kanamugire amesema kwamba gari hilo lilikamatiwa katika kata ya Rubengera. Na gari hiyo ni aina ya Fuso yenye nambari RAC 105 A, ilikuwa inaongozwa na Ntibakinze J. Bosco alikua akielekea katika kata ya Gishyita ambapo wanaweka vyuma vizee.

[ad id=”72″]

“kampuni hiyo ilikuwa imetoa mwito na kusema kwamba huibwa kila siku ndipo tulianza uchunguzi na raia wakatoa taarifa kwamba kuna gari ambalo hubeba vyuma vya mashini ambazo hutengeneza barabara, na hapo ndipo tukaandaa msako ili kuchunguza na vyuma hivyo tayari vimepewa tena kampuni yenyewe,” CIP Kanamugire alieleza.

CIP Kanamugire ametoa shukrani kwa raia ambao walitoa taarifa na kuwaomba kuwa makini ili kuchunguza mtu yeyote anayefanya kinyume na sharia ya nchi.

bonyeza hapa kupokea gazeti juu ya facebook juu ya twitter

Leki@bwiza.com

Leave A Reply

Your email address will not be published.

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.