kwamamaza 7

Polisi ya Rwanda yamrudishia raia wa Congo gari lake liliibiwa nchini Uganda

0

Raia wa jamhuri ya demokrasi ya Congo, Jean Marc Kasereka, jana alirudishiwa gari lake la aina ya Fuso ambalo liliibiwa nchini Uganda na kugunduliwa hapa Rwanda.

Lori yenye kuwa na nambari za Uganda, UAN 985X; iliibwa mnamo Julai 2016 na watuhumiwa wa kuiba lori hiyo waliingiza nchini Rwanda ndipo ilikamatwa na shirika za usalama.

Kamishina kaimu wa polisi ya kimataifa (Interpol) katika polisi ya Rwanda, ACP Peter Karake alieleza tukio na ushirikiano wa Interpol kwa kugundua majambazi hawa.

[xyz-ihs snippet=”google-pub”]

“Kasereka alinunua gari kutoka nchini Uganda, baadaye lilipotiwa kuibwa. Polisi ya kimataifa (Interpol) ya Uganda ilituita na tulikatiza lori kuingizwa nchini Congo.” Peter Karake alieleza.

Baada ya kurudishiwa gari lake, kasereka alishukuru polisi ya Rwanda. “Nashukuru sana polisi ya Rwanda (RNP) kwa namna walitatua kesi hii na kunipa gari langu.”

Zaidi ya magari 25 ya kigeni yalikatizwa na polisi ya Rwanda miaka ilipita. Magari mengi yalikuwa kutoka Kenya na yalirudishiwa wamiliki halali, wakati wezi walihamishwa katika nchi walifanyia dhambi.

bonyeza hapa kupokea gazeti juu ya facebook juu ya twitter

@Bwiza.com

Leave A Reply

Your email address will not be published.

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.