kwamamaza 7

Polisi ya Rwanda yafunguka kuhusu majigambo ya wanamgambo wa NLF

0

Polisi ya Rwanda imefunguka usalama umetiliwa mkazo karibu na mbuga ya Nyungwe ambako wanamgambo wa National Lieration Forces wanajigamba kutumia na kushambulia wilayani Nyaruguru,kusini mwa Rwanda.

Mkuu wa Polisi ya Rwanda, IGP Emmanuel Gasana amewaambia wakazi wilayani Nyaruguru  mashambulizi hayatatokea tena na kuhamasisha wakazi kuwasiliana vilivyo na wanausala kwa kupambana na suala  la watu wanaotaka kuharibu usalama wao.

“Hatuwezi kuvumilia yaliyotokea jana. Tuna imani kwamba hayatatokea tena,tunawataka nyinyi kuwasiliana vilivyo na wanausalama” IGP Gasana amesema

Mkuu wa Polisi ya Rwanda amefunguka haya baada ya  Kundi la wanamgambo kwa jina la National Liberation Forces (NLF) wamejigamba ndio waliofanya mashambulizi yote ya awali ambayo yaliua watu wawili na kuiba mali ya wakazi na kuwa wanalenga kuipindua serikali ya Rwanda.

NLF imetangaza ilishambulia pengi nchini Rwanda pakiwemo kusini mwa Rwanda,wilayani Nyaruguru, Cyangugu, Nyamagabe, Bugesera na Huye ambako ni kusini mwa Rwanda.

Hata hivyo,mashambulizi haya hayakujulikana katika vyombo vya habari na sisi hatuwezi kuhakikisha yalitokea.

Fred Masengesho Rugira/Bwiza.com

 

Leave A Reply

Your email address will not be published.

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.