Swahili
Home » Polisi ya Rwanda katika utumwa Centrafrika wamewapa mayatima msaada
HABARI

Polisi ya Rwanda katika utumwa Centrafrika wamewapa mayatima msaada

Askari polisi wa Rwanda 36 wenye kuwa katika utumwa wa amani katika nchi ya Central African Republic (CAR) wenye kuwa na lengo la kuchunguza kama huduma ya umoja wa mataifa huenda sawa, wamewapa mayatima wa nchi hiyo 36 msaada wa zawadi pakiwemo vifaa vya shule, usafi, vyakula na kazalika.

Tendo hilo kafanyika tarehe 15 April 2017 kwenye kikao cha kanisa la Ortodokse (Orthodox) sehemu ya Bimbo, na waliopewa ni watoto wenye umri kati ya miaka 3 na 5 wenye walifisha wazazi wao katika vita na wakishugulukiwa na uongozi wa kanisa hilo.

Katika ujumbe wao, kiongozi wa askari polisi kutoka nchi tofauti kwa ajili ya amani katika nchi hio, (Integrated Stabilization Mission in the Central African Republic (MINUSCA)), Brig Gen Roland Zamora, aliwashukuru polisi wa Rwanda kwa ajili ya tendo hilo, alisema ni tendo la kitofauti kwa ajili ya polisi wengine kutoka nchi zingine.

Eti,”hata wengine wakifanya kama hayo, sherti MINUSCA itawakumbuka daima, wakikumbuka kwamba ni mfano bora wa polisi ya Rwanda”.

Mpatanishi katika tendo hilo, Senior Superintendent of Police (SSP) Andrew Ndoli aliomba wakaaji wa sehemu hio ya Bimbo kujizulu na mabishano, aliwaomba kuwa na mila ya kusamehe na kutafuta maendeleo kamili.

Alisema tendo la kuwasaidia watoto mayatima ni kwa ajili ya kuwaonyesha upendo ya kuwa hata walipoteza wazazi, kuwa kuna familia pana ambayo inawajali na kuwajengea matumani ya siku za usoni.

[xyz-ihs snippet=”google”]

Walishiriki tendo hilo viongozi tofauti pakiwemo kiongozi wa jimbo la Ombella-M’Poko, Pierre Claver Zinga, kiongozi wa polisi ya Rwanda katika utumwa wa amani (FPU), Assistant Commissioner of Police (ACP) Elias Mwesigye.

bonyeza hapa kupokea gazeti juu ya facebook juu ya twitter

Leki@bwiza.com

Izindi wakunda

Tanga Igitekerezo

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.

Bwiza.com