Swahili
Home » Polisi ya Burundi yaishtumu ya Rwanda kumteka nyara mvuvi Mrundi
HABARI

Polisi ya Burundi yaishtumu ya Rwanda kumteka nyara mvuvi Mrundi

Polisi ya Burundi yawashtumu Polisi ya Rwanda kumteka nyara mvuvi mrundi aliyekuwa akivua katika mto wa Ruhwa, lakini mazungumzo ya kutolea suluhu tatizo hili yanaendelea.

Kwa mjibu wa Shirika la Utangazaji habari la Uchina Xinhua, mvuvi huu amekekuwa akivua katika mto wa Ruhwa uliyoko kwenye jimbo la Cibitoke ambapo ni mpaka wa Rwanda na Burundi Jumatano ya wiki hii,

Pierre Nkurikiye msemaji wa Polisi ya Burundi aliarifu kwamba mvuvi huyu anayetambulika kwa jina la Jackson Ndayikengurukiye amekamatwa Jumatano saa za saa moja na nusu za asubuhi.

Ameendelea kusema kwamba wanajeshi wa Rwanda waliwapiga risasi tano na kuwafanya wavuvi kukimbia sehemu tofauti huku mmoja akikimbilia Burundi na Jackson aliyekimbilia sehemu ya Rwanda akashikwa.

Hata hivyo Nkurikiye alisema kwamba mpaka sasa kunaendelea mazungumzo kuhusu suala hilo na kutafuta jinsi ya kumrudisha mvuvi huo Burundi.

Tatizo hili linafuatia shambulizi lililotekelezwa na watu wanaodhaniwa kutoka sehemu za Burundi na kumuua mtu 1 na wengine nane 8 kujeruhiwa kama ilivyotangazwa msemaji wa Jeshi la Rwanda.

bonyeza hapa kupokea gazeti juu ya facebook juu ya twitter

 Richard Wa Billy

Izindi wakunda

Tanga Igitekerezo

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.

Bwiza.com