Home HABARI Polisi walivamia mashabiki wa IS katika msikiti ulioko eneo la Moabit
HABARI - February 1, 2017

Polisi walivamia mashabiki wa IS katika msikiti ulioko eneo la Moabit

Polisi nchini Ujerumani hapo jana wamewatia mbaroni watu watatu wakihusishwa na kundi la itikadi kali linalojiita Dola la Kiislamu.

Vyombo vya habari nchini humo vimeripoti kuwa washukiwa hao walikuwa wanapanga shambulizi kubwa la kigaidi.

Aidha polisi walivamia msikiti mmoja ulioko katika eneo la Moabit mjini Berlin ambako watu hao wanadaiwa kuwa walikuwa wakikutana kwa mazungumzo.

Watu 12 waliuawa na wengine kadhaa kujeruhiwa Desemba 19 mwaka jana katika shambulizi linalodaiwa kufanywa na raia mmoja wa Tunisia Anis Amri baada ya kuendesha lori katika soko la Krismasi mjini Berlin lililokuwa limefurika watu hali iliyopelekea serikali ya Ujerumani kuchukua hatua za kuimarisha usalama.

[xyz-ihs snippet=”google”]

bonyeza hapa kupokea gazeti juu ya facebook juu ya twitter

@bwiza.com

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.