kwamamaza 7

Polisi wa Rwanda huko Haiti walivikwa medali ya shukrani

0

Askari polisi wa Rwanda wenye kuwa katika utumwa wa amani katika nchi ya Haiti (MINUSTAH) wajulikanao kama Individual Police Officers (IPOs), tarehe 21 April 2017 walivalishwa medali za shukrani kwa kazi yao.

Wamevalishwa na makamu wa mtume maalumu wa Umoja wa mataifa, El Moustafa Banlamlin.

Tendo hilo kafanyika katika mji mkuu wa nchi, Port Au Prince. Palikuwepo kiongozi wa MINUSTAH, Brig. Gen. Georges Pierre Monchette pamoja na kiongozi wa kundi la askari polisi wa Rwanda Murenzi Erc.

Banlamlin eti « munaonyesha juhudi na tabia nzuri siku kwa siku na hio huwapa usamini na pia husamini umoja wa mataifa, nafurahia jinsi munafanya kazi pamoja na wenzenu kutoka nchi tofauti ».

Kaendelea eti,”medali hizo munazo vikwa ni alama ya kuwa munafanya majukumu yenu vema, muendelee katika hali hio”.

Haiti, miaka nenda ilipatwa na mafuriko na upepo mwingi, askari polisi wa Rwanda walijitoa kwa kuwasaidia walio teseka, kujitoa huo kafurahisha viongozi wa nchi hata raia.

SP Murenzi eti:  « kuvikwa medali haiko usamini wetu pekee, ila ni usamini wa nchi yetu tunayo iwakilisha ».

[xyz-ihs snippet=”google”]

Alishukuru umoja wa mataifa kwa ajili ya medali hizo za shukrani, polisi ya Rwanda ilianza kuwatuma askari polisi katika utumwa wa amani huko Haiti mwaka wa 2010.

bonyeza hapa kupokea gazeti juu ya facebook juu ya twitter

@Leki/bwiza.com

Leave A Reply

Your email address will not be published.

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.