kwamamaza 7

Polisi Ufaransa wavunja kambi ya Calais

0

Ufaransa imeanza kubomoa mahema na vibanda katika kambi ya muda ya Calais iliyopewa jina la pori. Operesheni hiyo iliyoanza Jumatatu, ya kubomoa makaazi yaliyokuwa yakihifadhi wahamiaji wapatao 8,000, inatarajiwa kudumu kwa wiki nzima .

[ad id=”72″]

Katika siku ya kwanza, takriban watu wazima 2,000 na watoto 400 walihamishiwa katika maeneo tafauti nchini Ufaransa licha ya pingamizi kutoka kwa baadhi ya raia. Zaidi ya wahamiaji 1,636 walisajiliwa hapo jana, tayari kwa kuhamishwa katika makaazi mapya.

Idadi ya wahamiaji waliohamishwa tokea operesheni hiyo kuanza mwanzo mwa wiki imefika watu 4,014, kulingana na Waziri wa Mambo ya Ndani wa Ufaransa Bernard Cazeneuve.

[ad id=”72″]

Kwa wengi wa wahamiaji wanaotoka nchini Syria, Afghanistan na nyenginezo zinazokabiliana na migogoro, kufungwa kwa kambi ya Calais ndiyo mwisho wa ndoto yao ya kufika nchini Uingereza, ambayo ni jirani na mji huo wa bandari.
bonyeza hapa kupokea gazeti juu ya facebook na juu ya twitter
Bwiza.com

Leave A Reply

Your email address will not be published.

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.