Swahili
Home » Paul Kagame ameteuliwa kama mgombea rasmi na Chama chake cha RPF
HABARI MPYA SIASA

Paul Kagame ameteuliwa kama mgombea rasmi na Chama chake cha RPF

Wanachama wa RPF inkotanyi, katika mkutano wao mkuu wamemteua Paul Kagame kama mgombea atakae wania urais kwa tiketi ya RPF kwenye uchaguzi wa Agosti 2017.

Gasamagera Wellars, Kamshna wa Uhamsishaji katika chama cha RPF, kwa kuzingatia idadi ya wanachama wa ngazi za chini za uongozi waliomchagua kama mgombea, kwa niaba ya kamati ya uchaguzi wa chama cha RPF ametangaza rasmi kwamba Paul Kagame ndie atakaegombea kwa tiketi ya RPF katika uchaguzi wa rais utakaofanyika hapo tarehe 3 na 4 Agosti 2017.

Mkutano huu ulioendeshwa kwenye jengo jipya la Kifahari la RPF, umekuwa ukihudhuriwa na wanachama kutoka sehemu tofauti za nchi pamoja na wageni wasimamizi wa vyama kutoka pande tofauti za dunia ikiwemo ANC cha Afrika Kusini, CCM cha Tanzania, NRM cha Uganda , Communist Party cha Uchina na wengine kutoka nchi za Ethiopia, Angola, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo na Djibuti.

Hakukuwa na wagombea wenza waliojulikana kushindania tiketi hii kwa kuwa uchaguzi ulianzia kwenye ngazi ya kijiji na kila mwanachama mwenye kukidhi vigezo amekuwa akiruhusiwa kuwania tiketi hii.

Kumteua Paul Kagame kama mgombea kunafuatia referandamu ambayo ilifanyika mwaka wa 2016 na kuidinisha mabadiliko ya katiba katika ibara yake ya 101 na kumruhusu rais kuwania muhula mwingine.

[xyz-ihs snippet=”google”]

Wanyarwanda zaidi ya milioni 4 waliwasilisha nyaraka zao kwa bunge wakiomba mabadiliko ya katiba na walikuwa wakifanya hivi kwa sababu ya mafanikio aliyoyafikia Paul Kagame kama kusitisha mauaji ya Kimbari dhidi ya Watutsi, kuimarisha umoja na maridhiano ya wanyarwanda, kuukuza uchumi wa nchi na kuleta hali ya utiifu wa Rwanda kimataifa.

Kuteua kwa Paul Kagame kama mgombea kunafuatilia wagombea kama Dr Frank Habineza wa Green Party, Shima Rwigara Diane, Mwenedata Gilbert, Mpayimana Philippe na Barafinda Sekikubo Fred waliotangaza nia yao ya kuwania kiti cha urais iwapo watakubaliwa na Tume ya Uchaguzi.

bonyeza hapa kupokea gazeti juu ya facebook juu ya twitter

 Richard Wa Billy

 

Izindi wakunda

Tanga Igitekerezo

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.

Bwiza.com