kwamamaza 7

Paul Kagame aendesha kampeni zake wilaya ya Musanze,Nyabihu na Rubavu

0

Rais Kagame mgombea wa tiketi ya chama cha RPF amekuwa akiendesha kampeni zake wilaya za Musanze,Nyabihu na Rubavu ambako amesema kwamba umoja wao ndio unaowafanya wanyarawanda kulifikia kila lolote wanalolifikia.

 Kampeni za Kagame Musanze

Akiwasalimu

Rais kagame ambaye amekuwa wilaya ya Musanze na baadaye wilaya ya Nyabihu na Rubavu ambako wananchi wamekuwa wakimngojea kwa wingi amesema kufika kwao ni ishara ya umoja na nguvu zao,za RPF nguvu za kuijenga nchi.

Aliwaambia kwamba karibu kila lolote limekwisha na tarehe 4 Agosti itakuwa tu kama ishara na mambo yaendelee kwa kuijenga nchi kukijengwa shule,mabarabara na mengineyo.

[xyz-ihs snippet=”google”]

Hapa pia alipata fursa ya kuvipongeza vyama vilivyojiunga na RPF kwani ni ishara ya umoja wa wanyarwanda na kwamba ni chaguo nzuri lililowafanya wanyarwanda kuifikia hatua ambayo wamekwisha piga.

Amekamilisha hotuba yake kwa kuwashkuru na kuwaahidi kwamba atarudi baada ya uchaguzi kwa kuwashkuru baada ya uchaguzi mkuu.

 Kampeni za Kagame Rubavu na Nyabihu

Baadaye rais Kagame aliendelea na Kampeni zake Rubavu na Nyabihu ambapo wananchi wamekuwa wengi sana kama kawaida ya shughuli zake za kampeni kwenye wilaya zote alizokwisha zipitia.

Aliwakumbusha pia kwamba kura zao ndizo zitaamua ambalo wanyarwanda wanalolitaka. Akiwa wilaya ya Nyabihu alisema kwamba wanataka kuuondoa umaskini unaowakumba na kwamba pia maradhi inayotokana na ugonjwa wa kukosa chakula bora “kwashiorkor” hataki kamwe.

Alikamilisha hotuba kwa kuwashkuru na kuwahimiza kumpa kura zao

Baada ya hapo mgombea huu aliendelea na shughuli zake wilaya ya Rubavu ambapo amekuwa akisisitiza kwamba umoja na kushirikiana ndiyo nguzo ya maendeleo ya wanyarwanda.

Aligusia pia vyama nane vilivyoamua kujiunga na RPF na kumwunga mkono mgombea wake kwamba ndio ushirikiano unaotakiwa katika maendeleo ya Rwanda.

Aliwaambia kuwa maamuzi yao katika uchaguzi yategemea ikiwa wanataka umoja, maendeleo, Demokrasi vyote kwa kushirikiana.

 Bonyeza hapa kupata habari za hivi karibuni kwenye facebook na twitte

Richard Wa Billy

Leave A Reply

Your email address will not be published.

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.