kwamamaza 7

Papa Francis kuungwa mkono na waluteri licha ya ukosoaji kwa wakatoliki

0

Kiongozi wa kanisa katoliki duniani Papa Francis amekoselewa na wakatoliki wahafidhina kufuatia uamuzi wake wa kuhudhuria maadhimisho ya Jubilei ya miaka 500 ya mageuzi ya Kiluteri yaliyoanzishwa na Martin Luther yatakayofanyika nchini Sweden.

Martin Luther raia wa Ujerumani alianzisha mageuzi hayo mnamo mwaka 1517 mara baada ya kuandika tasnifu 95 akilikosoa kanisa katoliki la Roma kwa vitendo vya rushwa. Papa Francis anautembelea mji wa Lund kusini mwa Sweden ambako shirikisho la kiluteri la kidunia lilianzishwa mnamo mwaka 1947 na atafanya ibada ya pamoja na waluteri ili kuzindua maadhimisho hayo yatakayoendelea hadi mwakani.

Ziara ya kiongozi huyo inaonekana kuungwa mkono na waluteri licha ya ukosoaji kutoka kwa wakatoliki wahafidhina.

bonyeza hapa kupokea gazeti juu ya facebook juu ya twitter

@bwiza.com

Leave A Reply

Your email address will not be published.

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.