kwamamaza 7

Papa Francis awaita raia wa DRC kuwa vinara wa amani kwao

0

[ad id=”72″]

Kiongozi mkuu wa Kanisa Katoliki ulimwenguni Papa Francis leo amewatolea mwito raia wa Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo kuwa vinara wa amani, baada ya watu kuuawa katika maandamano dhidi ya kiongozi wa muda mrefu wa taifa hilo.

Papa Francis ameiambia hadhira ya kila wiki kuwa katika wakati huu nyeti katika historia ya taifa lao. Raia ya Congo wanapashwa kuwa vinara wa maridhiano na amani, na kuwasihi walioko katika nafasi za uongozi wa kisiasa kusikiliza sauti za dhamira zao, wajifunze kuona mateso ya raia wenzao na kutanguliza maslahi ya walio wengi.

Maaskofu wa kanisa katoliki wanaosimamia mazungumzo muhimu ya kutafuta suluhisho la amani nchini Congo wamesema makubaliano ni lazima yapatikane kabla ya sikukuu ya Krismass.

[ad id=”72″]

Mzozo umekuwa ukiongezeka nchini Congo kwa miezi kadhaa kuelekea muda wa mwisho wa Desemba 20 wa kumalizika kwa muhula wa pili na wa mwisho wa rais Joseph Kabila.

Kukiwa hakuna uchaguzi uliopangwa na hakuna dalili kwake kuachia madaraka, kiongozi wa muda mrefu wa upinzani Etienne Tshisekedi alitoa wito kwa raia milioni 70 wa taifa hilo kupinga kwa amani na kuukataa utawala wa Kabila.

Mazungumzo yalioanzishwa na kanisa katoliki wiki iliopita kutafuta suluhu ya mgogoro huo yalitarajiwa kuanza tena hii leo.

bonyeza hapa kupokea gazeti juu ya facebook juu ya twitter

[ad id=”72″]

Leki@bwiza.com

Leave A Reply

Your email address will not be published.

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.