kwamamaza 7

Papa Francis apiga marufuku ufanyabiashara ya sigara ndani ya Vatican mwaka ujao

0

Msemaji wa Vatican Greg Burke alisema kuwa mji huo mtakatifu hauwezi kukubali na kitendo ambacho kinahatarisha maisha ya binaadamu.

Takriban wafanyikazi 5000 wa Vatican na wale waliostaafu wanaruhusiwa kununua sigara zilizopunguzwa bei .

[xyz-ihs snippet=”google”]

Mauzo hayo yanakadiriwa kuiletea Vatican mamilioni ya yuro kila mwaka.

Lakini bwana Burke amesema kuwa hakuna faida ambayo ni halali iwapo sigara zinaathiri afya za wanaadamu.

[xyz-ihs snippet=”google”]

Alinukuu takwimu za shirika la afya duniani WHO ambazo zinalaumu uvutaji sigara kwa kusababisha vifo vya takriban watu miioni 7 duniani kila mwaka.

[xyz-ihs snippet=”google”]

”Nadhani watu wengi wanapenda sigara kwa sababu ya ufadhili wanaopata” ,alisema.

”Ni kitu ambacho ni lazima kufutilia mbali licha ya kuleta mapato Vatican, muhimu ni kufanya kile kilicho sawa”.

[xyz-ihs snippet=”google”]

Papa Francis ambaye pafu lake moja liliondolewa wakati alipokuwa kijana havuti sigara.

Wafanyikazi wa vatican na wale waliostaafu wanaruhusiwa kununua pakiti tano za sigara kila mwezi kutoka kwa duka lisilotozwa ushuru.

Chimbuko:BBC

Bonyeza hapa kupata habari za hivi karibuni kwenye facebook na twitter

Fred Masengesho Rugira/Bwiza.com

 

Leave A Reply

Your email address will not be published.

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.