kwamamaza 7

Orodha ya FIFA : Rwanda yashuka nafasi 10

0

Rwanda inazidi kushuka nafasi kwenye Orodha ya FIFA ikiwa inashika nafasi ya 128 ikifuatiwa na Nchi ya Afrika ya Kati ambayo, hivi karibuni watapambana katika michuano ya kutafuta tikiti ya kufuzu Michezo ya AFCON 2017.

 Rwanda ambayo inashika nafasi hii, imeshuka kutoka nafasi ya 118 mwezi uliopita hadi 128 ikiwa imekuwa na upungufu wa alama 39 hivi ikiwa na alama 246 kulingana na Orodha ya mwezi uliopita. Nchi ya Afrika ya Kati ambayo itakaribisha Rwanda tarehe 11 mwezi huu ndio inayofuata ikiwa nafasi ya 129 na ikiwa imesonga mbele nafasi moja kulingana na Orodha hiyo.

[xyz-ihs snippet=”google”]

Nchi nyingine za eneo la maziwa makuu ni pamoja na Congo DR inayokuja nafasi ya 39 na ikiwa imesonga mbele nafasi 2 nchi nyingine inayokuja karibu ni Uganda ikiwa nafasi ya 71 , Kenya nafasi ya 74 ikiwa imesonga mbele nafasi 4 huku Uganda ikisonga nafasi 1, Tanzania nafasi 139 ikipoteza nafasi 1 na Burundi ikiwa nafasi ya 148 ikiwa imepoteza nafasi 7 kulingana na Orodha ya mwezi uliopita.

Rwanda yazidi kushuka nafasi ikiwa miongoni mwa timu zilizopoteza nafasi nyingi kuliko nyingine kwenye Orodha hii, na inazidi kushushuka sana kwa kuwa ilikuwa nafasi ya 103 mwaka 2016.Pengine nchi ya Brazil ndiyo inashika nafasi ya 1 akiwa na alama 1715 ikifuatiwa na Arjentina na 1626, Ujerumani ikiwa ya tatu na alama 1511.

Nchi ya Afrika iliyoweza kuja nafasi ya karibu ni Misri ikiwa na alama   903, ikikaribiwa na Senega inayokuja nafasi 27 na alama 839.

bonyeza hapa kupokea gazeti juu ya facebook juu ya twitter

Richard Wa Billy/bwiza.com

Leave A Reply

Your email address will not be published.

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.