kwamamaza 7

Nyarugenge: Viongozi 4 wa kata wajiuzulu

0

Viongozi wa kata wanne kutoka wilaya ya Nyarugenge katika mji mkuu wa Kigali wamejiuzuru kwa sababu za kibinafsi, Meya amesema.

Viongozi hao ni Dusabumuremyi Innocent wa kata ya Kanyinya, Semitari Alexis wa kata ya Nyamirambo; Mutarugira Dieudonné wa kata ya Rwezamenyo na Bimenyimana Audace ambaye alikuwa kiongozi wa kata ya Mageragere.

Meya wa wilaya ya Nyarugenge Kayisime Nzaramba alithibitisha taarifa hii na aliambia Bwiza.com kwamba wamejiuzuru kwa sababu za kibinafsi.

[ad id=”72″]

“Ndio, viongozi hawa wameaga kwa sababu za kibinafsi. Hatuwezi kutoa maoni kwani kiongozi anapojiuzuru kwa sababu za kibinafsi ni uamuzi wa utashi wake”.

Viongozi wa serikali za mitaa hujiuzulu mfululizo wakisema kwamba ni sababu za kibinafsi ijapokuwa kuna wanaokamatwa na kupigwa jela baada ya siku chache kujiuzulu. Wiki hii viongozi wengine wawili wa kata ya Niboye na Gahanga walijiuzulu kutoka wilaya ya Kicukiro.

Theogene U @Bwiza.com

Leave A Reply

Your email address will not be published.

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.