kwamamaza 7

Nyanza:Ukiukaji wa haki za kujieleza watokomezwa

0

Hali ya ukandamizwaji na kunyimwa uhuru wa kujieleza imetoweka baada ya wakazi wa wilaya ya Nyanza kupata fursa ya kutoa maoni.

Mkazi wa kijiji cha Kirwa,Venancie Mukangarambe.

Baadhi ya viongozi wa ngazi za chini walikuwa wakilaumiwa kwa kutumia madaraka yao kama chanzo cha ubabe dhidi ya wananchi na kuwanyima uhuru wa kujieleza .

Hali ilivyo sasa ni tofauti kutokana na uhuru wa kujieleza kama wanavyoeleza  wananchi wilayani Nyanza.

[xyz-ihs snippet=”google”]

Bi Mkangarambe Venancie ni mkazi wa kijiji cha Kirwa ,kata ya Mshirarungu tarafa ya Bwabicuma wilayani Nyanza anasema kuwa kijijini

kwao kila mwananchi ana uhuru wa kujieleza na kutoa maoni pindi anapohitaji kufanya hivyo.

Raheri Nyirandayisaba  naye ni mkazi wa kijiji cha Kirwa. “Sisi tuna uhuru wa kutosha kabisa.Tunatoa mchango wetu na maoni bila kizuizi chochote.Na taarifa nyingi tunazipata pale tunapoenda kwenye mikutano ya Kata na hata kwenye usafi wa jumla” alisisitizia.

[xyz-ihs snippet=”google”]

Katika mahojiano na waandishi wa habari ,Mkuu wa wilaya ya Nyanza  Erasme Ntazinda alisema hakuna kiongozi wala mtu yoyote mwenye haki ya kuwanyima wananchi fursa ya kujieleza na hivyo haoni sababu ambayo itawafanya washindwe kutoa mchango wao katika masuala muhimu ya kimaendeleo wilayani humo.

“Wananchi wana uhuru wa kufikisha maoni yao na taarifa mbali mbali kupitia ujumbe mfupi (sms),na mara nyingine hutupigia simu na kutupatia taarifa mbalimbali”

Ameongeza kuwa wananchi hao hutoa taarifa na hata kusisitizia wasitajwe majina yao na kuongeza kuwa hatua hii ni nzuri na itasaidia katika masuala ya msingi ikiwa ni pamoja na vita dhidi ya rushwa.

[xyz-ihs snippet=”google”]

Erasme Ntazinda amesema juhudi za vyombo vya habari pia imesaidia kwa kiwango kikubwa kuwaelimisha wananchi kujua haki zao na uhuru wa kutoa maoni.

Hata hivyo bado kuna changamoto kutokana na baadhi ya wananchi kutotambua suala hili vema.

Bonyeza hapa kupata habari za hivi karibuni kwenye facebook na twitter

Hassan Thabiti/Bwiza.com

 

Leave A Reply

Your email address will not be published.

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.