kwamamaza 7

Nyamasheke:Mavazi ya kijana aliyetoweka yapatikana pwani ya ziwa Kivu

0

Mavazi yakiwemo suruali,viatu ya  kijana Jean Claude Sibomana,18, ambaye ni mkazi wa kijjii cha Amahoro,kata ya Nyamugari,tarafa ya Shangi,kusini magaharibi mwa nchi yamepatikana pwani ya ziwa Kivu baada ya siku nne  za kutoweka.

Taarifa hizi zimehakikishwa na kaka yake,Joseph Hakizimana alitoweka tarehe 23 Disemba 2017 alipoenda eneo la Nyabitekeri.

Nduguye amendelea kusema kuwa Sibomana alikuwa hana ugomvi na mtu yeyote kule kijijini kwao kwa kuwa alimaliza miaka mitatu akiishi mjini Kigali.

[xyz-ihs snippet=”google”]

Kiongozi wa wilaya ya Nyamasheke, Kamari Aime Fabien amefafanua kwamba taarifa hizi zimejulikana na kuwa polisi imeanza upelelezi husika na kisa hiki na kuwa mengi zaidi ya haya yatajulikana baada ya upelelezi.

Wanafamilia wametangaza kutokuwa na tumaini za kumuna akiwa hai.

Bonyeza hapa kupata habari za hivi karibuni kwenye facebook na twitter

Fred Masengesho Rugira/Bwiza.com

 

Leave A Reply

Your email address will not be published.

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.