kwamamaza 7

Nyamasheke: Viongozi wamaliza wasiwasi wa raia kuhusu upigaji kura

0

Raia wa Nyamsheke tarafa la Nyabitekeri wanalalamika kwa kutokuwa na kadi za uchaguzi na wakasema japokuwa wataruhusiwa kupiga kura bila kadi hawana uhakika kuwa hawatahitajika kuonyesha kadi hizo baadaye.

Wengi wa raia wa tarafa ya Nyabitekeri wakiwa katika mkutano wa umma wameonyesha wasiwasi wao, kwa viongozi waliokuwepo ambao ni katibu mtendaji wa tarafa, Uwimana Damas na katibu mtendaji wa wilaya ya Nyamasheke Kayumba Ephrem.

Félix Ndagijimana, raia wa kijiji cha Nyarusange, sehemu ya Mariba katika tarafa hiyi amesema kuwa wakati wa karibu aliokuwa na kadi ni katika mwaka wa 2003, kutoka hapo hajawahi kupatikana kwenye orodha ya kura, ila kuwekwa kwenye orodha ya nyongeza ili aweze kupiga kura.

“ni na wasiwasi kwamba kutokuwa na kadi ya uchaguzi ni kunyimwa baadhi ya haki zangu, ingawa nachaguwa haitoshi napaswa kuwa na kadi hiyo kama raia wengine. Sijihisi salama kuona wengine wakiwa na kadi wakati mimi nakuwa na kadi ya utambulisho” alisema

Mwingine aliyeonyesha wasiwasi wake ni Claude Ntakirutimana, ambaye anaishi kijiji cha Kamuhoza katika tarafa hii. Amesema kuwa ingawa amepoteza kadi yake ingepewa nyingine kwa kuwa anaona amenyimwa haki fulani na kusisitiza apewe”’

Katibu mtendaji wa Wilaya ya Nyamasheke,Kayumba Ephrem, alimaliza wasiwasi huu kwa kusema kuwa kutomiliki kadi ya Uchaguzi yaingekuwa pingamizi kwa kuwa kuna sheria maalum zinazohuso uchaguzi.

[xyz-ihs snippet=”google”]

Nibagwire Déo, mratibu wa Uchaguzi katika wilaya ya Nyamasheke na Rusizi, katika mahjiano na Bwiza.com alisema kwamba kutopatikana kwa Orodha ya Uchaguzi siyo pingamizi ya kumzuia mtu kupiga kura.

“Wawasiwe na wasiwasi wataweza kupiga kura, lakini kuhusu kadi nyingine za uchaguzi sidhani watapewa. Naelewa umuhimu wa kuwa na kadi ya uchaguzi, lakini mtu aliyeipoteza hatapewa nyingine bali kutatumiwa orodha ya nyongeza na kwa hivyo mtu ambaye hapatikani hata kwenye orodha ya nyongeza sidhani pia kuwa itawezekana kwake kupiga kura” Amesema

Tume ya Uchaguzi iliweka utaratibu wakujiandikisha kukitumiwa njia ya simu za mkononi na mtandao ambao watu walikuwa wanajiandikisha kwa madumuni ya kurahisisha na kuharakisha shughuli za kuwasajili wapigaji kura.

bonyeza hapa kupokea gazeti juu ya facebook juu ya twitter

 Richard Wa Billy

Leave A Reply

Your email address will not be published.

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.