kwamamaza 7

Nyagatare:Kiongozi ashtakiwa na wakazi kupokea frw 1000 ili kutoa huduma

0

Wakazi wa kata ya Rwimiyaga,tarafa ya Rwimiyaga wamemshitaki afisa wa kata kwa wajibu wa mambo ya kijamii, Jean Marie Vianney Ruyenzi kupokea frw 1000 kwa kila mkazi anayehitaji kujua ‘Ubudehe category’.

Wakazi wametangazia RBA kwamba huyu kiongozi anawaomba fedha  wanapokuenda kutafuta huduma za bima ya afya ‘mutuelle de Sante’.

“Mimi aliniomba kumpa hizi fedha nikamnyima,kwa hiyo sina bima ya afya.Anataka sisi tumpe frw 1000 ili kuchunguza kwenye tarakilishi kupitia mtandao ila viongozi wengine walikuwa wakitusaidia kupitia tarafa”mmoja mwa wakazi amesema

“Sisi wakazi tunampa kwa kuwa huwa tunahitaji bima ya afya lakini ni unyanyasaji kwa kuwa pengine hawalipi fedha hizi.Kuna wale ambao hawajapata bado bima ya afya kutokana na hili”mwingine ameongeza.

Jean Marie Vianney Ruyenzi amekanusha madai ya wakazi kwa kusema kuwa hawajawi kupokea fedha za wakazi kwa kuwapatia huduma.

Ruyenzi amesema”Sikubali kupokea frw1000, kila mtu husema yake kama kuna yule ambaye aliwahi kunilipa,ngali tayari kusikiliza ushahidi wake”.

Katibu mtendaji wa tarafa ya Rwimiyaga,Ruboneka Silva ameeleza kuwa hajui kuhusu suala hili ila hawezi kukana uwepo wake.

[xyz-ihs snippet=”google”]

“Kwa kawaida huduma hii hutolewa kwa bure,mala nyingi huduma hii hutolewa kwenye tarafa.Tutafanya ufuatiliaji wa jambo hili na adhabu itatolewa kulingana na sheria.

Katibu hali ameongeza kwamba Jean Marie Vianney  Ruyenzi ana makosa mengine ya kazi.

Subscribe to BWIZA TV to get news and song updates

Bonyeza hapa kupata habari za hivi karibuni kwenye facebook na twitter

Fred Masengesho Rugira/Bwiza.com

 

Leave A Reply

Your email address will not be published.

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.