kwamamaza 7

Nyagatare: Bomu lawaua wachungaji wa ng’ombe tano

0

Wachungaji wa ng’ombe tano waliuawa jana na mlipuko wa bomu wilayani Nyagatare. Tukio lilifanyikiwa mwituni karibu na kambi la majaribio la jeshi la Rwanda, Gabiro.

Inasemekana kwamba waathirika hawa walilipiga bomu hilo baada ya kulipata ijapokuwa shirika za usalama zinasema kama hazijagundua habari kamili kuhusu sababu ya kulipuka kwa bomu hio.

Msemaji wa polisi ya Rwanda, ACP Theos Badege alithibitisha taarifa hii na kusema kwamba wachungaji hawa waliuawa na bomu jana mchana.

[ad id=”72″]

‘’Ilifanyika jana,  walikuwa wachungaji wa ng’ombe. Baada ya habari kusambaa, shirika za usalama na raia walienda na kuwakuta wachungaji wamefariki kunabaki vifaa vyao tu.’’ ACP Badege alisema.

Msemaji wa polisi aliwaomba raia na wazazi kuwaonya watoto kutowasiliana na mambo wasiolewa.

bonyeza hapa kupokea gazeti juu ya facebook juu ya twitter

@Bwiza.com

Leave A Reply

Your email address will not be published.

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.