Ladislas Ntaganzwa aliyekuwa kiongozi wa wilaya (commune) ya Nyakizu mwaka wa 1994, tarehe 30 Mach 2017 aliambiwa makosa tano kuhusu mauaji ya Kimbari na anasema ya kwamba yale ambayo wataonyesha dalili atakubali.

Ntaganzwa anashutumiwa mauaji ya Kimbari, uhamasishaji wa Mauaji ya Kimabri, kuongoa kabila, kuua na kuzini kwa makazo.

Uendesha mashtaka ulisoma kwanza anwani ya Ladislas Ntaganzwa aliye tiwa mbaroni akiwa katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, husema kwamba alikuwa kiongozi wa MDR-Power huko Nyakizu na alikuwa akitoa msaada kwa wauguzi (Assistant Medical) katika kundi la wapiganaji wa FDLR Foca msituni Congo.

Alisema kuwa anwani ni yake ila anasema kwamba hakuelewa mashtaka kwa sabau yaliandikwa kwa lugha ya kingereza, lugha ambayo haifahamu.

[xyz-ihs snippet=”google”]

Ntaganzwa alipo ulizwa kama atasamba akikubali au kukana, alisema kwamba hana mengi ya kusema kwa sababu kuna tatizo litokanalo na lugha asiyo ifahamu, eti “jinsi itakuwevyo nikiona kuna dalili nitakubali”.

Uendesha mashtaka walipo pewa muda walisema ya kwamba Ntaganzwa alitumikisha madaraka aliyokuwa nayo kama kiongozi wa wilaya kwa kutoa shurti ya kumaliza Watusi na kutiwa katika matendo kwa sababu walikuwa wakitii asemalo.

Husema kuwa tarehe 7 April 1994, watusi walitoka jimbo la Gikongoro na Butare wakikimbilia katika wilaya ya Nyakizu iliyo ongozwa na Ladislas Ntaganzwa na wengi wao wakakimbilia katika parokia Cyahinda ambapo walifikilia hifadhi ndani ya nyumba ya Mungu.

Ntaganzwa pia alizunguka sehemu nyingi akihamasisha watu kukimbilia parokia ili waweza kuwalindia usalama na walikubali haraka kwa sababu ni kiongozi asemavyo.

Mwendesha mashtaka eti “ila haikukuwa hivyo kwa sababu lengo ilikuwa kuwakusanya nafasi moja na kuwaua bila kuwakuta nyumbani kwao”.

Uendesha mashtaka husema kwamba tangu tarehe 7 hadi 15 April 1994 kwenye parokia hio kulikimbilia Watusi wapatao 30.000 na walikuwa wakishambuliwa ili kuwamaliza.

Ushuhuda husema kuwa Ntaganzwa aliongoza shambulio mara nyingi pakiwemo shambulio la tarehe 15 yenye jeshi, polisi na Interahamwe. Husema pia kuwa Ntaganza alikuwa nasilaha naye alipiga lisasi wamoja na walio tafuta kukimbia walikamatwa na wakaaji wahutu na kuwaua kupitia silaha ya kiasili.

[xyz-ihs snippet=”google”]

Mshutumiwa husema pia kuwa ndie alianzisha shambulio la parokia ya Cyahinda na kuongoza shambulio la sehemu ijulikanayo kwa jina la “Ibisi bya Nyakizu (Gasasa)” na Watusi 7000 waliokimbilia sehemu hio waliuawa. Ntaganzwa alikuwa akivaa nguo za askari jeshi na alikuwa na silaha.

Ntaganzwa anashutumiwa kuongoza mikutano ya uhamasishaji wa kumaliza Watusi kama mkutano wa tarehe 7 April 1994, ambamo watu walipewa majukumu ya kuongoza uuaji. Alipana silaha za kufanyisha mauaji. Atafikishwa tena mahakamani tarehe 6 April.

Wanaopendelea bwiza.com iwatembelee na kuwatangazia habari kwenye bidhaa vyao wanaweza kutumia ujumbe kwenye barua pepe ya meckypro@gmail.com, ama wapigie simu kwenye nambari ifuatayo: 0784685981.

bonyeza hapa kupokea gazeti juu ya facebook juu ya twitter

Leki@bwiza.com

ACHA JIBU

Tanga igitekerezo
Andika amazina

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.