kwamamaza 7

Norway: Mnyarwanda akamatwa kwa kutuhumiwa mauaji ya kimbali

0

Serikali ya Norway imetangaza Mnyarwanda ambaye majina yake hayakutangazwa amekamatwa jumanne juu ya kutuhumiwa kushiriki katika mauaji ya kimbali dhi dhidi ya Tutsi mwaka 1994.

Ofisi ya upelelezi nchini humo ‘Kapros’ imeeleza mtuhumiwa alikamatwa alipokuwa mjini Nohland na kufungwa mwezi kizuizini bila yeyote kumtembelea.

“Kuna sababu kamili za huyu kutuhumiwa mauaji ya kimbali hasa Watutsi”

Mtuhumiwa alifika nchini Norway kama mkimbizi mwaka 2006 na kupatiwa uraia mwaka 2014.

Mwendeshamashtaka Espen Hanken ametangaza Polisi ilifanya  utafiti husika na mtuhumiwa mala tatu mwaka 2017 na kuwakuta washahidi kuhusu uhalifu wa mtuhumiwa.

Huyu amesisitiza upelelezi wa haya mashtaka  utaendelea.

Norway ni  baadhi ya nchi ambazo zinawakamata na kuwahukumu watuhumiwa wa mauaji ya kimbali dhidi ya Tutsi mwaka 1994

Fred Masengesho Rugira/Bwiza.com

Leave A Reply

Your email address will not be published.

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.